DR. SAMIA - JUMBE HOLIDAY BONANZA LAMALIZIKA KWA KISHINDO


Mdau wa michezo Mhandisi James Jumbe (katikati) akiendesha baiskeli.
Mdau wa michezo Mhandisi James Jumbe (katikati) akiendesha baiskeli.
Mdau wa michezo Mhandisi James Jumbe akikabidhi zawadi kwa washindi.

Picha zote na Marco Maduhu

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Sherehe za mapumziko ya mwisho wa mwaka na kuukaribisha mwaka mpya 2025 maarufu kama DR. SAMIA / JUMBE HOLIDAY BONANZA 'Shinyanga Imeamka!', zilizofanyika katika mji wa Shinyanga, zimefungwa kwa kishindo. 

Bonanza hili  lililoandaliwa na Mdau wa michezo, Mhandisi James Jumbe, limejumuisha mashindano ya michezo mbalimbali na zawadi nono kwa washindi, ikiwa ni pamoja na fedha taslimu, ng'ombe, kuku, soda, na mchele.

Mashindano ya DR. SAMIA / JUMBE HOLIDAY BONANZA yamejumuisha michezo mingi ya aina mbalimbali, kama vile mpira wa kikapu, bao, karata, drafti, msusi mwenye kasi zaidi, mbio za baiskeli, netball, wavu, PS Game, mchezo wa kufukuza kuku, kushindana kula, pull table, na muziki, ambapo washiriki wamepata fursa ya kuonyesha vipaji vyao na kushindana kwa furaha na mshikamano.

Michezo mingine imejumuisha mechi za soka, ambapo timu za Bodaboda FC na Bajaji FC zilikutana, na Bajaji FC kuibuka washindi. Timu ya Rangers FC ya wilaya ilikutana na Ngokolo FC, ambapo Ngokolo FC walishinda, huku DERBY ya Upongoji (Upongoji Sports Club na Upongoji Stars) ikiisha kwa mikwaju ya penati.

Bonanza hili limefanyika katika Viwanja vya CCM Kambarage, Mjini Shinyanga, na mchezo wa mwisho, mpira wa kikapu, unafanyika usiku wa mkesha katika Viwanja vya Risasi, ambapo umati mkubwa wa watu umekusanyika kuupokea mwaka mpya.

Mhandisi Jumbe amesema kuwa amefarijika kuona muitikio mkubwa wa wananchi wa Shinyanga kushiriki katika michezo mbalimbali. 

Amesisitiza kuwa lengo la mashindano haya ni kuonyesha vipaji vya vijana wa Shinyanga na kuhamasisha michezo katika mkoa.

“Lengo letu ni kuona vijana wetu wanapata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao na kupata nafasi ya kuendelezwa. Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan anahimiza michezo, na kupitia mashindano haya, tunataka kukuza michezo na vipaji katika mkoa wetu,” amesema Mhandisi Jumbe.

Aidha, Mhandisi Jumbe amesisitiza umuhimu wa michezo kwa jamii, akisema, “Michezo ni ajira, inaimarisha afya, inadumisha amani, mshikamano, na kuleta umoja. Pia, michezo ni njia nzuri ya kupunguza stresi na burudani kwa vijana wetu.”

Katika ujumbe wake wa kuhitimisha mwaka 2024, Mhandisi Jumbe ameahidi kufanya mambo makubwa zaidi mwaka 2025, ikiwemo kuleta matamasha ya muziki na mashindano ya kombe la mpira wa pete, akiahidi kuzialika timu kutoka wilaya jirani.

Baadhi ya washiriki wa bonanza hili wametoa shukrani kwa Mhandisi Jumbe kwa kuunga mkono sekta ya michezo, na kueleza kuwa mashindano kama haya ni fursa muhimu kwa vijana kupata ajira na kukuza vipaji vyao.

Mdau wa michezo Mhandisi James Jumbe akizungumza kwenye bonanza hilo.
Mdau wa michezo Mhandisi James Jumbe akikabidhi zawadi kwa washindi.
Ng'ombe , zawadi za washindi.
Ng'ombe , zawadi za washindi.
Mdau wa michezo Mhandisi James Jumbe akisalimiana na wachezaji.
Michezo ikiendelea.
Mashindano ya kula.
Mashindano ya kunywa juice.
Mratibu wa bonanza la michezo Dr.Samia /Jumbe Holiday Jackline Isaro akicheza bao.
Mashindano yakiendelea.
Mbio za baiskeli.
Mshindano ya Polltable.

Picha zote na Marco Maduhu
Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA