WAANDISHI WA HABARI WATEMBELEA MRADI WA UKARABATI NA UPANUZI WA KIWANJA CHA NDEGE CHA SHINYANGA

 Muonekano sehemu ya barabara ya ndege katika Kiwanja cha Ndege Shinyanga

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Waandishi wa habari kutoka Mkoa wa Shinyanga, kupitia Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club - SPC), wamefanya ziara ya kushuhudia maendeleo ya mradi wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Shinyanga.

 Mradi huu unaotarajiwa kukamilika ifikapo Aprili 1, 2025, unafadhiliwa na serikali ya Tanzania na unajengwa na Mkandarasi wa China, Hennan International Corporation Group Co. Ltd (CHICO), kwa gharama ya shilingi bilioni 49.18.

Ziara hiyo imefanyika leo, Desemba 23, 2024, ambapo waandishi wameshuhudia hatua kubwa za maendeleo katika ujenzi wa mradi huu muhimu. Muonekano sehemu ya barabara ya ndege katika Kiwanja cha Ndege Shinyanga

Kwa mujibu wa Msimamizi Mwakilishi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Chiyando Matoke, ujenzi umefikia hatua nzuri, ikiwa ni pamoja na kukamilika kwa barabara ya ndege (runway). 

Amesema hadi sasa, mradi umefikia asilimia 80 ya utekelezaji wake, na sehemu kubwa iliyobaki ni ujenzi wa jengo la abiria, ambalo bado linaendelea.

Mhandisi Matoke ametoa shukrani kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujitolea kuboresha miundombinu nchini, akisema kuwa ujenzi huu ni sehemu ya dhamira yake kubwa ya kuhudumia taifa.

 Ameongeza kuwa serikali tayari imeshalipa fedha zote za mradi huo, na ahadi ya kukamilika kwa wakati bado ipo imara.

Mhandisi Chiyando Matoke, akielezea kuhusu hatua iliyofikiwa mradi wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Shinyanga 

Kwa upande wake, Mhandisi Ruburi Kahatano, Mhandisi wa Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege Shinyanga, amesisitiza kuwa atasimamia utekelezaji wa mradi huu ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati na kulingana na vigezo vya mkataba.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) , Greyson Kakuru, ameeleza kuwa kukamilika kwa mradi huu kutakuwa ni mwanzo wa safari mpya ya ukuaji wa uchumi katika Mkoa wa Shinyanga. 

Kakuru amesema kuwa uboreshaji wa miundombinu ya usafiri, ikiwemo Kiwanja cha Ndege cha Shinyanga, utaleta manufaa makubwa kwa wakazi wa mkoa na taifa kwa ujumla.

Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Shinyanga ni mradi wa kimkakati utakaosaidia kuimarisha usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo, na kuchangia katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa mkoa na nchi kwa ujumla.
Msimamizi Mwakilishi wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Chiyando Matoke, akielezea kuhusu hatua iliyofikiwa mradi wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Shinyanga wakati Waandishi wa habari kutoka Mkoa wa Shinyanga walipofanya ziara katika Kiwanja hicho kilichopo Ibadakuli Mjini Shinyanga - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Msimamizi Mwakilishi wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Chiyando Matoke, akielezea kuhusu hatua iliyofikiwa mradi wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Shinyanga 
Mhandisi wa Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege Shinyanga Ruburi Kahatano akielezea kuhusu ujenzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Shinyanga 
Mhandisi wa Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege Shinyanga Ruburi Kahatano akielezea kuhusu ujenzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Shinyanga 
Mhandisi wa Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege Shinyanga Ruburi Kahatano akielezea kuhusu ujenzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Shinyanga 
Mhandisi wa Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege Shinyanga Ruburi Kahatano akielezea kuhusu ujenzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Shinyanga 
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (SPC) , Greyson Kakuru akizungumza wakati waandishi wa habari wakitembelea ujenzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Shinyanga 
Meneja mradi wa ukarabati na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Shinyanga , Kampuni ya CHICO, Shi Yinlei akizungumza wakati wa ziara ya waandishi wa habari
Msimamizi wa ujenzi wa jengo la abiria Kiwanja cha ndege Shinyanga, Mhandisi Fatuma Iddi Mruma akizungumza wakati wa ziara ya waandishi wa habari
Afisa Usalama wa Kiwanja cha Ndege Shinyanga, Jeremiah Kileo akizungumza wakati wa ziara ya waandishi wa habari
Viongozi mbalimbali wanahusika na ujenzi wa Kiwanja cha Ndege Shinyanga wakiwaongoza waandishi wa habari kutembelea kiwanja cha ndege Shinyanga
Viongozi mbalimbali wanahusika na ujenzi wa Kiwanja cha Ndege Shinyanga wakiwaongoza waandishi wa habari kutembelea kiwanja cha ndege Shinyanga
Viongozi mbalimbali wanahusika na ujenzi wa Kiwanja cha Ndege Shinyanga wakiwaongoza waandishi wa habari kutembelea kiwanja cha ndege ShinyangaViongozi mbalimbali wanahusika na ujenzi wa Kiwanja cha Ndege Shinyanga wakiwaongoza waandishi wa habari kutembelea kiwanja cha ndege ShinyangaMuonekano sehemu ya jengo la abiria linaloendelea kujengwa katika Kiwanja cha Ndege ShinyangaMuonekano sehemu ya jengo la abiria linaloendelea kujengwa katika Kiwanja cha Ndege ShinyangaMuonekano sehemu ya barabara ya ndege katika Kiwanja cha Ndege Shinyanga
Muonekano sehemu ya barabara ya ndege katika Kiwanja cha Ndege Shinyanga
Viongozi mbalimbali wanahusika na ujenzi wa Kiwanja cha Ndege Shinyanga wakiwaongoza waandishi wa habari kutembelea kiwanja cha ndege Shinyanga
Viongozi mbalimbali wanahusika na ujenzi wa Kiwanja cha Ndege Shinyanga na waandishi wa habari wakipiga picha ya kumbukumbuViongozi mbalimbali wanahusika na ujenzi wa Kiwanja cha Ndege Shinyanga na waandishi wa habari wakipiga picha ya kumbukumbu

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA