Na Gustaphu Haule, Pwani
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kupitia Jumuiya ya Wazazi Hamoud Jumaa( MNEC), amesema kuwa miaka minne ya uongozi wa Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan imekuwa na mafanikio makubwa kwa Taifa na Wananchi wake.
Jumaa amesema mafanikio hayo yametokana na sera na mikakati ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo imekuwa ikilenga kuongeza ushirikiano na maendeleo ya jamii kwa ujumla.
Kauli hiyo ya Jumaa imekuja ikiwa ni sehemu ya kumpongeza Rais Samia kwa kazi alizofanya katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake tangu aliporidhi kiti hicho kutoka kwa mtangulizi wake Hayyati John Pombe Magufuli (JPM) aliyefariki Machi 2021.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamoud Jumaa (MNEC) katikati akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka (kushoto) na Kulia ni Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa.
Jumaa amesema kwa maoni yake Rais Dkt. Samia amefanikiwa kutokana na kusimamia mambo makubwa manne ambayo kimsingi yamesaidia kuleta tija na faida kwa Watanzania na Taifa nzima kiujumla.
Jumaa, ametaja jambo la kwanza kuwa ni ushirikiano katika jamii, ambapo amesema Serikali imehamasisha ushirikiano wa jamii katika maamuzi yanayohusu maendeleo ya elimu,afya na miundombinu.
Amesema jambo hilo ,limewapa Wazazi na wanajamii nafasi ya kutoa maoni na kushiriki katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao bila kushurutishwa wala kulazimishwa.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamoud Jumaa (MNEC) kulia akizungumza na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Mohamed Mchengerwa
(kushoto)
Jumaa, amesema jambo la pili ni kuimarisha miundombinu,ambapo Rais Samia amefanikiwa katika ujenzi na uboreshaji wa vituo vya afya na Shule hasa katika maeneo yasiyopatikana huduma bora.
Amesema, katika suala la kuimarisha miundombinu imesaidia jamii kupata huduma bora za afya na elimu na kwamba imechangia kuboresha maisha ya kila siku ya Wananchi.
Jambo la tatu, ni kuwezesha kiuchumi,Jumaa amesema kuwa Rais Samia amekuwa na dhamira ya dhati ya kuwainua kiuchumi Wananchi wake na katika kudhihirisha hilo amerudisha mikopo isiyokuwa na riba sambamba na kuendesha programu mbalimbali za ujasiriamali.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamoud Jumaa (MNEC) Kulia akiteta jambo na Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani Kite Mfilinge(kushoto)
Amesema kuwa,katika hilo Rais Samia ametoa fursa kwa jamii kujitegemea kiuchumi ambapo imewasaidia wazazi, Wanawake na Vijana kujenga biashara ndogondogo na kuboresha hali ya maisha.
Jumaa ametaja jambo la nne kuwa ni Kukuza Maadili na Umoja wa Jamii ambapo Rais Samia ameanzisha program za elimu ya maadili na nidhamu ambazo kwa kiasi kikubwa zimejikita katika kuimarisha uhusiano na umoja katika jamii.
Amesema suala la maadili na umoja limewasaidia wazazi na watoto kuishi katika mazingira yenye heshima , ushirikiano na jamii.
Hatahivyo,Jumaa amesema kwa ujumla juhudi hizo zinaongeza ushawishi wa Jamii katika kufanya maamuzi muhimu na kuchangia katika maendeleo endelevu huku zikisaidia kujenga jamii yenye ustawi wa kijamii na uchumi.
Club News Editor
Comments
Popular posts from this blog
RC PWANI AONGOZA WAKAZI PWANI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA
Na Gustaphu Haule, Pwani MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amewaongoza wakazi wa Mtaa wa Mkoani" A" uliopo Kata ya Tumbi Halmashauri ya Mji Kibaha katika zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura lililoanza leo Mkoani Pwani. Aidha, Kunenge akiwa katika kituo hicho aliambatana na Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Rashid Mchatta, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson Saimoni pamoja na mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Rogers Shemwelekwa. Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akiwaongoza Wananchi wa Mtaa wa Mkoani "A", Kata ya Tumbi Halmashauri ya Mji Kibaha kujiandikisha katika daftari la wapiga kura zoezi ambalo limeanza leo Oktoba 11 hadi Oktoba 20 mwaka huu Akizungumza mara baada ya kujiandikisha katika kituo hicho Kunenge amesema kuwa zoezi hilo limeanza kufanyika Mkoa wa Pwani leo Oktoba 11 na litamalizika Oktoba 20 mwaka huu. Kunenge amesema kuwa kufanyika kwa zoezi hilo ni maandalizi ya kuelekea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia ...
MAGUMU YA JOSEPHINE GUNDA NA HARAKATI ZA UDIWANI VITIMAALUM KIBAHA VIJIJINI.
Na Gustaphu Haule,Pwani UNAPOWATAJA Madiwani wa Viti maalum Mkoa wa Pwani hutakosa kumtaja Josephine Gunda diwani wa viti maalum anayetokea katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Vijijini. Josephine ambaye ni Mkazi wa Kata ya Kwala na mama wa watoto watatu alianza harakati za Kisiasa mwaka 2010 kwenye kinyang'anyiro cha kuwania udiwani wa viti maalum. Kwasasa Josephine ni awamu yake ya tatu kushika nafasi hiyo tangu alipoanza kuchaguliwa mwaka 2010,2015 na 2020 kupitia Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Kibaha Vijijini. Katika mahojiano na Mwandishi wa makala haya Josephine anasema kuwa awali kabla hajaingia katika kisiasa alikuwa kiongozi wa moja ya kanisa lililopo nyumbani kwake Kwala. Sio uongozi wa kanisa tu,lakini amewai kuwa kiongozi wa masuala ya kijamii akifanyakazi na Shirika la Camfed lililokuwa linashughulika na elimu kwa wanafunzi wakike Kibaha Vijijini. Anasema ,kilichomvutia kuingia katika Siasa ni baada ya kuona viongozi wa kisiasa namna wanavyoweza kuku...
MWEKEZAJI GARDEN KIBAHA MJINI AMLILIA RC KUNENGE
Na Mwandishi Wetu,Kibaha MWEKEZAJI wa eneo maarufu la Garden lililopo Kata ya Tumbi katika Halmashauri ya Mji Kibaha Zakaria Jensen amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge kumsaidia kutatua changamoto zinazomkabili ili haweze kufanya biashara yake katika mazingira mazuri . Jensen,amesema kwasasa anafanya biashara zake kwa mashaka makubwa kutokana na baadhi ya watendaji kutoka katika Halmashauri hiyo kutaka kumuondoa kinguvu katika eneo hilo bila kupewa sababu ya msingi. Anasema,anachokishangaa kuona baadhi ya watendaji wa Halmashauri wakifanya njama za kumuondoa wakati yeye amepangishwa eneo hilo na Wakala wa barabara Mkoa wa Pwani (Tanroads). Eneo la garden lililopo Kata ya Tumbi katika Halmashauri ya Mji Kibaha lililowekewa alama nyekundu ya x inayomtaka mmiliki wake Zakaria Jensen kubomoa kama linavyoonekana pichani. Amesema, eneo la Kibaha Mailimoja na eneo la Tumbi lililopo kando ya barabara ya Morogoro ni eneo la Tanroads na kuna wafanyabiashara zaidi ya 3000 ambao ...
Post a Comment