
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
WAUMINI wa Dini ya Kiislamu,wamesisitizwa kuendelea kutenda mema kama walivyokuwa wakifanya kwenye mfungo wa Ramadhani.

Hayo yamebainishwa leo Machi 31 na Sheikh wa wilaya ya Shinyanga Soud Kategile, wakati akitoa hutoba mara baada ya Swala ya Eid kumalizika,iliyo ongozwa na Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya,katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Shinyanga.
Amesema mfungo wa Ramadhani kumalizika siyo ndiyo watu watende mambo mauvo, na kuwasihi kwamba ni vyema wakaendelea kuishi kwa kutenda mambo yaliyomema pamoja na kufuatilia na kusoma mafundisho ya Mwenyezi Mungu.

“Baada ya Ramadhani kuisha,nawaombeni sana waumini wa dini ya Kiislamu muendelee kutenda mema, pamoja na kufuatilia na kusoma mafundisho ya Mungu kama iliyokuwa wakati wa Mfungo,”amesema Sheikh Kategile.
Katika hatua nyingine amewasihi Watanzania, kwamba katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa kuchagua Madiwani,Wabunge na Rias wawe makini kwa kuchagua viongozi wapenda maendeleo na kujali matatizo ya watu,na siyo kuwachagua wale watoa fedha.

Nao baadhi ya waumini hao,waliwasihi wenzao kwamba wakasherehekee sikukuu hiyo ya Eid pamoja na familia zao, na siyo kwenda kutenda mambo ya Anasa.
TAZAMA PICHA👇👇

Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Mkusanya akiongoza Swala ya Eid.

Sheikh wa wilaya ya Shinyanga Soud Kategile akitoa hotuba kwenye Swala ya Eid.






Post a Comment