DKT. TULIA APEWA TUZO YA HESHIMA KUTAMBUA MCHANGO WAKE KWA JAMII


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ametunukiwa Tuzo ya Heshima ya Malkia wa Nguvu kutoka Clouds Media Group, ikiwa ni kutambua mchango wake mkubwa kwa jamii pamoja na Uongozi wake uliomfikisha kuwa Rais wa IPU.


Tuzo hiyo imetolewa usiku wa tarehe 5 Aprili, 2025, katika kilele cha Hafla ya Tuzo za Malkia wa Nguvu iliyofanyika jijini Dar es Salaam.


Dkt. Tulia ametambuliwa kwa namna ya kipekee kutokana na juhudi zake za kuhamasisha wanawake na wasichana nchini kujiamini, kujituma na kupambana bila kuchoka ili kufanikisha ndoto zao.


Kwa niaba ya Mhe. Dkt. Tulia, tuzo hiyo imepokelewa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Zainab Katimba.

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA