"HAKUNA WA KUZUIA UCHAGUZI" MBUNGE KISHOA APINGA VIKALI "NO REFORM NO ELECTION"



 Na Robert Onesmo

Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Singida ,Mhe Jesca David Kishoa amepinga vikali kampeni ya NO REFORM NO ELECTION inayofanywa na Chama Cha Demokrasia na maendeleo[CHADEMA]kikishinikiza uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kutokufanyika mpaka pale serikali itakapofanya mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi.

 


Kishoa amezungumza hayo April .5 .2025 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Mwanga iliyopo wilaya ya Mkalama Mkoani Singida,ambapo amesema kwa jeshi lililopo la ulinzi na usalama hakuna wa kuzuia uchaguzi kwani limejipanga kikamilifu.

 

“Kwa jeshi hili lililopo hapa la ulinzi na usalama kuna mtu atazuia uchaguzi huu?jeshi limejipanga na liko imara, nawashukuru sana viongozi wa jeshi la Polisi”

 


Vile vile MHE. Jesca Kishoa amesema kuwa anaamini katika uchaguzi mkuu ambao utafanyika mwaka Mkoa wa Singida kupitia wilaya ya Mkalama itampa kura za kutosha Rais Samia kwa kazi kubwa alioifanya.

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA