SAASHISHA AIBUA UPYA SAKATA LA WAWEKEZAJI WASIO NA UWEZO HAI, SERIKALI YATOA KAULI NZITO


Na, Mwandishi wetu Fichuzi news blog- Dodoma.


Kutokana na mikakati mbalimbali inayotekelezwa na serikali ambayo inalenga kuwawezesha wananchi kukua kiuchumi wakiwemo wananchi wa Wilaya ya Hai,  serikali imeendelea kuhakikisha mradi wa kiwanda cha KMTC unatekelezwa ambapo Serikali kupitia Halmashauri hiyo imetenga eneo malumu la uwekezaji lenye ukubwa wa hekta 463 ambalo linaendelea kutangazwa kwa wawekezaji mbalimbali.


Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Stanslaus Haroon Nyongo kufuatia swali la Msingi la Mbunge wa Jimbo la Hai Mhe. Saashisha Elinikyo Mafuwe alilouliza kuwa "Je, Serikali ina mpango gani wa njia mbadala ya kukuza uchumi wa Wananchi wa Hai kutokana na uhaba wa ardhi ya uzalishaji." Leo Aprili 8, 2025 katika bunge la kumi na mbili Mkutano wa kumi na tisa Kikao cha kwanza Jijini Dodoma.


"Kwa upande wa Wilaya ya Hai, serikali imeendelea kuhakikisha mradi wa kiwanda cha KMTC unatekelezwa. Aidha, Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Hai imetenga eneo malumu la uwekezaji lenye ukubwa wa hekta 463 ambalo linaendelea kutangazwa kwa wawekezaji mbalimbali, Hivyo, serikali itaendelea kuhimiza na kutangaza fursa zinazopatikana katika Wilaya ya Hai ikiwemo fursa za Utalii ili kuimarisha uchumi wa wananchi." Amesema Naibu Waziri huyo


Naibu Waziri ameainisha mikakati hiyo kuwa ni pamoja na Kutoa Mikopo yenye riba nafuu hususani kwa wanawake, vijana na walemavu, Kujenga mfumo wa kidijitali vijijini ili kuongeza Matumizi ya TEHAMA katika shughuli za kiuchumi, na Kuweka mazingira wezeshi ya kuvutia uwekezaji, hasa katika sekta ya viwanda. 


Kufuatia majibu hayo ya serikali mbunge huyo akauliza maswali ya nyongeza yaliyolenga uwepo wa tathimini ya ardhi ya mashamba yote 17 ili mikataba watakayoingia ihusanishe thamani ya ardhi iliyopo, huku swali la pili akielezea sababu inayofifisha uchumi wa Jimbo la Hai ni wawekezaji wasio na uwezo wanaoingia mikataba na mashamba hayo ya ushirika likiwemo shamba la Makoa lililopo kijiji cha Uduru ambalo shughuli zake zimesimama kwa takribani miaka minne kutokana na mwekezaji huyo kuwa na migogoro isiyoisha na kutolipa chochote n.k.


Hata hivyo Naibu Waziri Nyongo ameweka wazi kuwa Serikali katika bajeti ya mwaka huu imebainisha kuweka mkakati mkubwa wa kwenda kufanya tathmini ya kina ya mali zote ambazo ziko chini ya TR na mali zote za serikali ili kujua dhamani na iwe rahisi mikataba watakayoingia iwe yenye tija na manufaa na keshi ambazo ziko mahakamani ziweze kuchukuliwa hatua stahiki.


Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA