WIZARA YA NISHATI YAOMBA BAJETI YA TSH. TRILIONI 2.246


Na, Mwandishi wetu Fichuzi news blog - Dodoma.

Serikali kupitia Wizara ya Nishati imeliomba bunge kuidhinisha bajeti ya mwaka wa fedha 2025/26 jumla ya Shilingi Trilioni Mbili, Bilioni Mia Mbili Arobaini na Sita, Milioni Mia Saba Arobaini na Tano, Mia Nne Arobaini na Tano Elfu (Shilingi 2,246,745,445,000) kwa ajili ya matumizi ya Wizara hiyo na Taasisi zake.


Hotuba hiyo ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa mwaka 2025/2026 imewasilishwa na Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko  bungeni jijini Dodoma leo April 28, 2025.


"Naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu sasa liidhinishe Bajeti ya jumla ya Shilingi Trilioni Mbili, Bilioni Mia Mbili Arobaini na Sita, Milioni Mia Saba Arobaini na Tano, Mia Nne Arobaini na Tano Elfu (Shilingi 2,246,745,445,000) kwa ajili ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake. Mchanganuo wa fedha hizo ni Shilingi Trilioni Mbili, Bilioni Mia Moja Sitini na Saba, Milioni Mia Tano Kumi na Tatu, Mia Mbili Kumi na Tisa Elfu (Shilingi 2,167,513,219,000) sawa na asilimia 96.5 ya Bajeti yote ya Wizara ni kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo. Kati ya fedha hizo, Shilingi Trilioni Moja, Bilioni Mia Nne Sitini na Sita na Milioni Ishirini, Mia Mbili Sabini na Nne Elfu (Shilingi 1,466,020,274,000) ni fedha za ndani na Shilingi Bilioni Mia Saba na Moja, Milioni Mia Nne Tisini na Mbili, Mia Tisa Arobaini na Tano Elfu (Shilingi 701,492,945,000) ni fedha za nje" na

 

"Shilingi Bilioni Sabini na Tisa, Milioni Mia Mbili Thelathini na Mbili, Mia Mbili Ishirini na Sita Elfu (Shilingi 79,232,226,000) sawa na asilimia 3.5 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya fedha hizo Shilingi Bilioni Sitini na Tisa, Milioni Mia Tisa Thelathini na Mbili, Mia Tatu na Sita Elfu (Shilingi 69,932,306,000) ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC) na Shilingi Bilioni Tisa, Milioni Mia Mbili Tisini na Tisa, Mia Tisa Ishirini Elfu (Shilingi 9,299,920,000) ni kwa ajili ya Mishahara (PE) ya Watumishi wa Wizara na Taasisi ya PURA." Amesema Dk. Biteko.    




Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA