Wabunge bunge la Jamhuri ya Muungno wa Tanzania wameanza kuijadili hotuba iliyotolewa na rais wakati kifungua bunge la kumi na moja ambapo mgogoro wa Zanzibar umeibua mjadala miongoni mwao huku wengine wakitaka serikali iingiliye kati na wegine wakisema kwa sasa serikali haipaswi na haina mamlaka ya kufanya hivyo.
Kabla ya wabunge kuanza kuchangia hotuba hiyo Mh waziri mkuu Kassim Majaliwa aliwataka wabunge kutumia hotuba hiyo kama njia sahihi ya kutoa ushauri na mapendekezo ya namna ambavyo serikali inaweza kuboresha utendaji wake.
Mh. Abdalah Mtolea ni mbunge kutoka chama cha wananchi CUF akiwakilisha jimbo la Temeke amesema Dk Magufuli anatakiwa kuingilia kati mgogoro wa Zanzibar kwani suala hilo lipo ndani ya mamlaka yake.
Mh Joseph Msukuma ni mbunge wa CCM jimbo la Geita yeye anapingana vikali na mawazo hayo na kusema kwa sasa suala hilo linasubiri uchaguzi na siyo maamuzi ya rais Dk Magufuli.
Mbali na mgogoro wa Zanzibar Mh John Heche amesema hotuba ya rais haina jambo lolote jipya ni hotuba kama hotuba zingine ambazo wananchi wamekuwa wakizisikiliza kila rais mpya anapoingia madarakani.
Wakati mbunge huyo akitoa kauli hiyo Mh George Lubeleje kutoka Mpwapwa na Mh Asha Abdalah Juma kutoka Zanzibar wamesema hotuba hiyo ni dhira muhimu kwao.
إرسال تعليق