Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara imeliomba Bunge kuidhinisha kiasi cha shilingi Bilioni 119 ikiwa ni makadirio ya Mapato na Matumizi Kwa mwaka wa Fedha 2023/2024.
Ni kufuatia hotuba yaWaziri wa
Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji ambapo ameliomba Bunge kuidhinisha kiasi cha shilingi 119,017,998,000 na kuwa
kati ya fedha hizo, shilingi 75,451,494,000 ni matumizi ya kawaida
ambapo shilingi 63,086,267,000 ni mishahara na shilingi 12,365,227,000
ni matumizi mengineyo.
Dkt. Kijaji amesema shilingi
43,566,504,000 zinaombwa kwa ajili ya matumizi ya maendeleo ambapo
shilingi 30,346,819,000 ni fedha za ndani na shilingi 13,219,685,000 ni
fedha za nje.
إرسال تعليق