Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini Mhe. Joseph Kasheku 'Msukuma' ameitaka Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Kuwa na tabia ya Kusikiliza Changamoto za wafanyabiashara na kumaliza matatizo yao ili waweze kufanya biashara zao kwa Uhuru.
Ameyasema hayo Leo tarehe 4 mwezi wa 5 mwaka 2023 wakati akichangia hotuba liyowasilishwa na Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Ashatu Kijaji bungeni jijini Dodoma.
"Kuweni na Tabia ya kuwasikiliza watu na Kumaliza matatizo hatuna sababu ya kuja kupigizana kelele, Wala hatuhitaji tutajane na kama Kuna mtu Yuko nyuma ya huu mchezo amekula vya kutosha, Fanyia kazi matatizo ya wafanyabiashara Ili muweze kuendana na Kasi ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia" Alisema Mhe. Msukuma
"Barua tunazo hapa kiswahili tu Come torrow! Come tomorrow wafanyabiashara mwisho wake wanasema Kuna mtu nyuma yake Haiwezekani Wafanyabiashara wamekuja kwako na wamesha kaa vikao zaidi ya kumi ugumu uko wapi wa kutoa maamuzi? tuambie nani Yuko nyuma ya huu mchezo?" Alisema Mhe. Msukuma
Post a Comment