SAKATA LA TANGA CEMENT LAPAMBA MOTO "HAIWEZEKANI KUNA MTU YUKO NYUMA YA HILI" MBUNGE MSUKUMA

 


Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini Mhe. Joseph Kasheku 'Msukuma' ameitaka Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Kuwa na tabia ya Kusikiliza Changamoto za wafanyabiashara na kumaliza matatizo yao ili waweze kufanya biashara zao kwa Uhuru.

Ameyasema hayo Leo tarehe 4 mwezi wa 5 mwaka 2023 wakati akichangia hotuba liyowasilishwa na Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Ashatu Kijaji bungeni jijini Dodoma. 

"Kuweni na Tabia ya kuwasikiliza watu na Kumaliza matatizo hatuna sababu ya kuja kupigizana kelele, Wala hatuhitaji tutajane na kama Kuna mtu Yuko nyuma ya huu mchezo amekula vya kutosha, Fanyia kazi matatizo ya wafanyabiashara Ili muweze kuendana na Kasi ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia" Alisema Mhe. Msukuma

"Barua tunazo hapa kiswahili tu Come torrow! Come tomorrow wafanyabiashara mwisho wake wanasema Kuna mtu nyuma yake Haiwezekani Wafanyabiashara wamekuja kwako na wamesha kaa vikao zaidi ya kumi ugumu uko wapi wa kutoa maamuzi?  tuambie nani Yuko nyuma ya huu mchezo?" Alisema Mhe. Msukuma

Kufuatia hilo ukaibua mjadala wa sakata la TAANGA CEMENT na Kiwanda cha Chalinze jambo ambalo ameonyesha kuwa na wasiwasi nalo.

"Sheria mbovu ndizo zinazotufukuzia wawekezaji, swala la TANGA CEMENTI Kuna mchezo tunachekechwa aidha humu ndani au huko nje Kuna mtu pia yuko nyuma" Mhe. Msukuma

 "Waziri ukija hapa uje na majibu mazuri tusije tukaharibu Image ya nchi yetu kwa wahuni wanatembea na briefcase kwenye kwapa, hatuwezi kuishi kwa dilidili,  Huyo Chalinze ni nani? tusitembezwe dili humu ndani, mnajenga tabia mbaya, Hawa wacheza dili tutangazie hicho kiwanda cha Chalinze kiko wapi?" Mhe. Msukuma


"Mshindani wako unamwoneaje wivu kufilisika? mpaka ukafungue kesi umeona wapi hii kama Sheria tulitunga mbovu tuacheni kutembea na dili kwapani jamani tutetee Tanzania" Mhe. Msukuma


Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA