BARRICK BULYANHULU YAFIKISHA KAMPENI YA USALAMA YA ‘JOURNEY TO ZERO’ KWENYE JAMII

 


Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Cheick Sangare,akiongea na wananchi wakati wa mafunzo hayo ya usalama kwa jamii.

Baadhi ya waendesha punda za kubeba mizigo kutoka vitongoji mbalimbali wilayani Msalala wakifurahia na viongozi wao na wafanyakazi wa Barrick baada ya kukabidhiwa zawadi ya jaketi za kinga ya ajali (Reflector) wakati wa mafunzo ya uhamasishaji usalama kwa jamii yaliyoandaliwa na mgodi wa Barrick Bulyanhulu.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Cheick Sangare,akitoa zawadi ya jaketi la kinga ya ajali (Reflector) kwa mmoja wa waendesha punda za kubeba mizigo wakati wa mafunzo ya uhamasishaji usalama kwa jamii yaliyoandaliwa na kampuni hiyo na kufanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kakola wilayani Msalala jana.
***
Katika jitihada za kuhakikisha jamii inakuwa salama,Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kupitia kauli mbiu yake ya kuhamasisha usalama ya Journey to Zero imeshirikiana na Jeshi la Polisi kutoa mafunzo ya usalama katika jamii wilayani Msalala mkoani Shinyanga.

Mafunzo hayo yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi ya Kakola yalihusisha viongozi wa vijiji na kata mbalimbali, wananchi, wanafunzi na waendesha pikipiki na mifugo ya kubebea mizigo.

Katika mafunzo hayo yaliyoendeshwa na Maofisa kutoka Jeshi la Polisi na wataalamu wa usalama kutoka Mgodi wa Bulyanhulu wananchi walipata elimu kuhusiana na usalama barabarani, kukabiliana na majanga ya moto pia waendesha pikipiki na wanyama wa kubeba mizigo waligawiwa jaketi maalumu (Reflectors) kwa ajili ya kuwawezesha kuonekana kwa urahisi wanapotembea usiku ili wasigongwe na magari.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu, Cheick Sangare, alisema Usalama ni suala ambalo kampuni ya Barrick inalipa kipaumbele kikubwa na ndio maana imeamua kuandaa programu za kuelimisha jamii kuzingatia usalama lengo kubwa likiwa ni kutokomeza vitendo hatarishi kwa usalama wa wananchi.

Sangare, alisema ili kufanikisha suala hili ni jukumu la kila mmoja kuzingatia kujilinda na kuwalinda wenzake sambamba na kuhakikisha anapinga na kukemea matukio yanayoweza kusababisha matukio ya ajali.

”Barrick kupitia kauli mbinu yetu ya Journey to Zero tutaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali za kutokomeza matukio ya ajali nchini” ,alisema.

Akiongea kwa niaba ya viongozi wa vijiji na madiwani kutoka kata mbalimbali waliohudhuria katika mafunzo hayo,Diwani wa kata ya Bugarama, Prisca Msoma, aliishukuru Barrick Bulyanhulu, kwa kuja na programu ya kuelimisha jamii masuala ya usalama kuanzia wa barabarani hadi majumbani sambamba na kugawa vifaa vya kujikinga na ajali katika makundi mbalimbali kwajamii.

“Kupitia Programu hii ya kuelimisha jamii masuala ya usalama,Barrick mmedhihirisha kuwa mnawajali wananchi katika jamii,kwa maana usalama ni suala la msingi kwa kila mtu na alitoa wito kwa wananchi kuzingatia mafunzo waliyoyapata pia alitoa wito kwa madereva kuanzia wa magari ,Pikipiki na wanyama wanaobeba mizigo kuzingatia usalam na kufuata alama za usalama barabarani”,alisema Msoma.


Kwa upande wake Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Msalala,Elias Msome, alisema Jeshi hilo litaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wanaounga mkono jitihada za kutokomeza ajali na aliwahimiza wananchi kuzingatia kanuni za usalama wakati wote ili kufanikisha mkakati wa Serikali wa kuhakikisha matukio ya ajali zisizo za lazima zitokanazo na uzembe yanatokomezwa.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria mafunzo hayo katika jukwaa kuu
Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Msalala,Elias Masome akiongea na wananchi wakati wa mafunzo hayo.
Diwani wa Kata ya Bulyanhulu,Shija Luyombya akitoa shukrani kwa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kuunga mkono jitihada za Serikali za kuendesha mafunzo ya usalama barabarani.
Mrakibu Msaidizi wa Polisi wilayani Msalala,John Kahibi akielezea matumizi ya alama za barabarani na sheria za barabarani kwa wananchi waliohudhuria mafunzo hayo.
Mtaalamu wa zimamoto kutoka mgodi wa Barrick Bulyanhulu Eric Chacha, akitoa mafunzo ya kuzima moto.
Baadhi ya waendesha punda za kubeba mizigo kutoka vitongoji mbalimbali wilayani Msalala wakifurahia zawadi za jaketi za kinga ya ajali (Reflector) walizozawadiwa na Barrick Bulyanhulu wakati wa mafunzo hayo.
Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA