Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini , Mhe. Fue Mrindoko akikagua ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule ya msingi Msufini kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga
Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini imeeleza kusikitishwa na matofali yanayotumika kujenga vyumba vitatu vya madarasa na matundu matatu ya vyoo katika shule ya Msingi Msufini kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga kwamba ziko chini ya viwango.
Akizungumza wakati wa ziara ya kamati hiyo ikitembelea na kukagua ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo katika shule hiyo leo Jumamosi Mei 2023, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Mhe. Fue Mrindoko amesema kamati hiyo imebaini matofali hayo hayana kiwango kwani mengine wameyaona yakiwa na matope/udongo unaopukutika.
"Matofali haya hayana kabisa kiwango na ujenzi unaendelea sasa hatuelewi next (baadaye) itakuwaje katika madarasa na vyoo hivi vinavyojengwa...si yatabomoka kabla ujenzi haujaisha??", amesema Mrindoko.
"Kutokana na matofali haya kuwa chini ya kiwango tunaona kabisa tutajenga mara mbili...Niwaombe sana wanaohusika wafahamishwe haraka, haiwezekani matofali yapo chini ya kiwango namna hii halafu ujenzi unaendelea...Hayana kiwango kabisa, pembeni kuna saruji ndani kuna udongo unamong'onyoka kwa vidole...Kamati ya utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi CCM Shinyanga Mjini imeona Matofali haya haya kiwango kabisa, yaondolewe hatuwezi kujenga mara mbili", ameongeza Mrindoko.
Mrindoko amewashukuru walimu wa shule hiyo kuona mapungufu ya matofali hao na kutoa taarifa mapema ili kuepuka majanga yanayoweza kujitokeza hapo baadaye.
“Tumesikitishwa kuona matofali haya yanayotumika yapo chini ya kiwango. Tunaziomba mamlaka zinazohusika zije kukagua ujenzi huu na kuangalia namna ya kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza. CCM haiwezi kukubali fedha zinazotolewa na serikali zitumike vibaya”,ameongeza Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Yotham Kibabi.
Akisoma taarifa ya ujenzi huo Mwalimu Mkuu msaidizi wa Shule ya Msingi Msufini kata ya Ndala , Godfrey Oscar Jebele amesema madarasa hayo matatu na matundu matatu ya vyoo yanajengwa kupitia mradi wa BOOST na umeanza Mei 15,2023 ukiwa na gharama ya shilingi 84,600,000 (Milioni 84.6).
“Changamoto iliyopo katika ujenzi huu ni kwamba mafundi wanalalamika kuwa tofali zinazotumika baadhi zinakuwa na changamoto kwani zinapukutika”,amesema Jebele.
Diwani wa kata ya Ndala Zamda Shaban amesema haiwezekani mradi huo uharibiwe hivyo atahakikisha changamoto hiyo inatatuliwa.
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini wakiangalia matofali yanayotumika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika shule ya msingi Msufini kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Mei 20,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini , Mhe. Fue Mrindoko akiangalia matofali yanayotumika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika shule ya msingi Msufini kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini , Mhe. Fue Mrindoko akizungumza katika shule ya msingi Msufini kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga
Matofali yanayotumika katika ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo katika shule ya msingi Msufini kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga.
Matofali yanayotumika katika ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo katika shule ya msingi Msufini kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga.
Matofali yanayotumika katika ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo katika shule ya msingi Msufini kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini , Mhe. Fue Mrindoko akikagua ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule ya msingi Msufini kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini , Mhe. Fue Mrindoko akikagua ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule ya msingi Msufini kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga
Wajumbe wa kamati ya utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini wakikagua ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule ya msingi Msufini kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga

Ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule ya msingi Msufini kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga ukiendelea
Diwani wa kata ya Ndala Zamda Shaban akizungumza wakati Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini ikifanya ziara kwenye kata hiyo
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Yotham Kibabi akizungumza katika kata ya Ndala
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini , Mhe. Fue Mrindoko akizungumza katika kata ya Ndala
Mwalimu Mkuu msaidizi wa Shule ya Msingi Msufini kata ya Ndala , Godfrey Oscar Jebele (kulia) akikabidhi taarifa ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo katika shule hiyo kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini , Mhe. Fue Mrindoko
Ujenzi wa madarasa ukiendelea katika shule ya msingi Msufini kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga.
Ujenzi wa madarasa ukiendelea katika shule ya msingi Msufini kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga.
Wajumbe wa kamati ya utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini wakikagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya CCM Kata ya Ndala

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Yotham Kibabi akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Ndala
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Yotham Kibabi akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Ndala
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga Mjini , Mhe. Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM kata ya Ndala

إرسال تعليق