Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, John Tesha akiwapatia watoto zawadi ya juisi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani katika Manispaa ya Shinyanga
Mtoto Catherine James akitoa neno la shukrani kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi kuadhimisha siku ya familia duniani katika kituo cha Buhangija.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imeadhimisha Siku ya Familia Duniani katika Kituo cha Kulelea Watoto wenye Mahitaji Maalumu cha Buhangija pamoja na kutoa zawadi kwa watoto na akina mama katika Wodi ya Wazazi Kituo cha Afya Kambarage ambapo Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi amesisitiza wajibu wa usimamizi wa familia ni kila mmoja ili kuimarisha maadili na upendo kwa familia imara.
Maadhimisho ya Siku ya Familia katika Manispaa ya Shinyanga yakiongozwa na Kauli mbiu ya Mwaka 2023 "Imarisha Maadili na Upendo kwa Familia Imara" yamefanyika leo Jumatatu Mei 15,2023 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, Mhe. Samizi ili kuwa na familia zenye maadili na upendo serikali inapendekeza wanafamilia (Baba, Mama, Watoto,ndugu na jamaa wa karibu) kukaa pamoja ili kujadili mafanikio katika familia na kupongezana, lakini pia kujadili changamoto zilizopo ili kutafuta majawabu ya pamoja kwa amani na upendo ili kuendelea kudumisha mshikamano na maelewano ndani ya familia na jamii yote kwa ujumla.
“Katika Manispaa yetu ya Shinyanga maadhimisho haya ya Siku ya Familia Duniani yatukumbusha wazazi na walezi wajibu wetu wa msingi wa malezi ya watoto na familia hasa kwa akina baba kujua wajibu wao kama wazazi au walezi kwa Watoto katika maeneo makuu 3 ya msingi ambayo ni kumjali mtoto katika maeneo ya msingi, kumlinda mtoto dhidi ya ukatili na kuzungumza na mtoto mara kwa mara ili kufahamu changamoto zinazomkabili na maendeleo yake kwa ujumla”,amesema Mhe. Samizi.
“Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Familia duniani mwaka 2023 isemayo "Imarisha Maadili na upendo kwa familia imara" inatumika kuwakumbusha wazazi na walezi umuhimu wa maadili mema na upendo miongoni mwa wanafamilia. Inazikumbusha familia umuhimu wa kuzingatia maadili mema ya Kitanzania katika malezi na makuzi ya watoto wetu”,amefafanua Mkuu huyo wa wilaya.
Ameongeza kuwa kauli mbiu hiyo pia inasisitiza upendo ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima inayopelekea familia nyingi kusambaratika na kuacha watoto bila uangalizi wa pamoja hivyo kukosa huduma muhimu.
“Familia ni chanzo cha jamii yoyote duniani,kwa kuwa kila mtu amezaliwa na amekulia katika Taasisi hii muhimu katika jamii. Familia inaundwa na Mume, Mke na Watoto na katika utamaduni wetu ndugu wa karibu wanakuwa sehemu ya familia. Majukumu ya familia ni pamoja na kutoa huduma muhimu zikiwemo mahitaji ya Watoto na familia, ulinzi na mawasiliano”,ameeleza.
“Siku ya familia inatoa fursa pia kujadili haki za kila mwanafamilia bila kujali hali yake ikiwemo watoto wenye ulemavu wa kila aina hata wa ngozi ambao katika sehemu nyingi hasa barani Afrika wamekuwa waathirika kiasi cha kupindukia kutokana na kasumba mbaya za ushirikina”,ameongeza Mhe. Samizi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akimpa zawadi ya sabuni mama kwenye wodi ya wazazi katika Kituo cha Afya Kambarage wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani katika Manispaa ya Shinyanga.
Hata hivyo Mhe. Samizi amesema changamoto kubwa katika kukabiliana na ukatili dhidi ya watoto ni ukimya unaotawala kwenye familia nyingi katika kutoa taarifa za vitendo vya ukatili vinavyofanyika ndani ya familia hii ikiwemo kuepuka kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mkosaji, mila na desturi,kuwepo kwa imani potofu zenye madhara zinazotekelezwa katika baadhi ya familia, uelewa mdogo kuhusu malezi chanya na mawasiliano duni miongoni mwa wanafamilia.
Aidha amesema ukosefu wa kipato au umaskini miongoni mwa familia zimepelekea wazazi na walezi wengi kutotimiza majukumu yao ya Msingi ya malezi.
“Hali hii ya umsakini imepelekea watoto wengi kujiingiza kwenye vitendo visivyofaa katika jamii, ikiwa pamoja na kuongezeka kwa utoro shuleni, kuongezeka kwa vitendo vya ukatili na maambukizi ya VVU”,amesema.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (kushoto) akiwapatia watoto zawadi ya juisi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani katika Manispaa ya Shinyanga
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga John Tesha ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii amesema tarehe 15 Mei ya kila mwaka ni Siku ya kimataifa ya Familia, ambayo ilizinduliwa rasmi na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 1989 kwa lengo la kutoa kipaumbele juu ya masuala yote yanayohusu familia na jamii.
“Tumekutana hapa kwa ajili ya kukumbushana masuala ya familia ikizingatia hivi sasa tunakabiliwa na tatizo la malezi ambapo kuna mmomonyoko wa maadili. Ni jukumu letu sote kuhakikisha familia inakuwa katika maadili.
Maafisa maendeleo ya jamii wetu wanaendelea kutoa elimu ili kuhakikisha matukio ya ukatili wa kijinsia yanayotokana na ukosefu wa maadili katika familia na jamii kwa ujumla yanatokomezwa”,amesema Tesha.
Naye Mkuu wa Shule ya Msingi Buhangija Jumuishi ambaye ni Msimamizi wa Kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalumu cha Buhangija Bi. Fatuma Gilalah amesema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 967 kati yao wenye mahitaji maalumu ni 194 kati ya wenye ulemavu wa viungo ni 16, wasioona 30, viziwi 84, wenye ualbino 78 na mmoja mwenye uoni hafifu.
Tangu tarehe 15 Mei 1989 hadi 15 Mei 2023 ni miaka 34 tangu Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa ulipoweka Siku ya Kimataifa ya Família.
Umoja wa Mataifa umetenga siku hii kwa ajili ya kutoa fursa ya kuchagiza uelewa wa masuala yanayoath familia ikiwemo kijamii kiuchumi na kidemografia.
Kutokana na umuhimu wa familia kama chanzo cha jamii, Baraza kuu la usalama na Umoja wa Mataifa kupitia tamko Na. 4//23/ la tarehe 20 Mei la mwaka 1993 lilipitisha siku hii kuwa siku maalum kwa ajili ya kutathmini hali za familia na maendeleo yao.
Tanzania ikiwa ni miongoni mwa wanachama wa Umoja wa Mataifa iliridhia na imekuwa ikifanya Maadhimisho ya siku ya familia kwa kuratibu shughuli mbalimbali zinazohusu maendeleo ya familia.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani katika Manispaa ya Shinyanga yaliyofanyika leo Jumatatu Mei 15,2023 katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija Mjini Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani katika Manispaa ya Shinyanga yaliyofanyika leo Jumatatu Mei 15,2023 katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija Mjini Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani katika Manispaa ya Shinyanga yaliyofanyika leo Jumatatu Mei 15,2023 katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija Mjini Shinyanga
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, John Tesha akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani katika Manispaa ya Shinyanga yaliyofanyika leo Jumatatu Mei 15,2023 katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija Mjini Shinyanga
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani katika Manispaa ya Shinyanga yaliyofanyika leo Jumatatu Mei 15,2023 katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija Mjini Shinyanga
Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Buhangija Jumuishi Fatuma Gilalah akitoa taarifa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani katika Manispaa ya Shinyanga yaliyofanyika leo Jumatatu Mei 15,2023 katika kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija Mjini Shinyanga
Mwenyekiti wa Mtaa wa Bugwandege kata ya Ibinzamata Amani Abdalah akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani katika Manispaa ya Shinyanga
Mtoto Catherine James akitoa neno la shukrani kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi kuadhimisha siku ya familia duniani katika kituo cha Buhangija.
Watoto wakitoa burudani ya wimbo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani katika Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (kushoto) akiwapatia watoto zawadi ya juisi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani katika Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (kushoto) akiwapatia watoto zawadi ya juisi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani katika Manispaa ya Shinyanga
Maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani katika Manispaa ya Shinyanga yakiendelea
Maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani katika Manispaa ya Shinyanga yakiendelea
Maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani katika Manispaa ya Shinyanga yakiendelea
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akiagana na watoto wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani katika Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akiagana na watoto wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani katika Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza na akina mama katika Kituo cha Afya Kambarage wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani katika Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza na akina mama akizungumza na mama kwenye wodi ya wazazi katika Kituo cha Afya Kambarage kisha kukabidhi zawadi ya sabuni wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani katika Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akimpa zawadi ya sabuni mama kwenye wodi ya wazazi katika Kituo cha Afya Kambarage wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani katika Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akimpa zawadi ya sabuni mama kwenye wodi ya wazazi katika Kituo cha Afya Kambarage wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani katika Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akipiga picha na vingozi mbalimbali wa Manispaa ya Shinyanga wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani katika Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akipiga picha na vingozi mbalimbali wa Manispaa ya Shinyanga wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani katika Manispaa ya Shinyanga.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
إرسال تعليق