Maafisa Wahifadhi wa TAWA kutoka Pori la Akiba Muhesi wamefanikiwa kumuokoa mtoto wa tembo anaekadiriwa kuwa na umri wa kati ya wiki 2 au 3 aliyetumbukia katika kisima cha maji kitongoji cha Ipunguli, Kijiji cha Doroto Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Mtoto huyo wa tembo aliyekuwa amepoteana na kundi la wazazi wake alitumbukia kisimani katika harakati za kuwatafuta wazazi wake.
Baada ya zoezi la kumuokoa mtoto huyo wa tembo Mei 23, 2023, Maafisa Wahifadhi wa TAWA walimpatia huduma ya kwanza, Kwa kumpa maziwa na kulitafuta kundi la wazazi wake na hatimaye kumuunganisha pamoja nalo.
Hii ni mojawapo ya kazi za Maafisa na askari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kuhakikisha wanalinda na kuokoa maisha ya Wanyamapori Kwa faida ya kizazi kilichopo na vizazi vijavyo Ili waweze kufaidi urithi wa Nchi yao na kutekeleza Kwa vitendo Kauli Mbiu ya Wizara ya Maliasili na Utalii isemayo "Tumerithishwa...Tuwarithishe"
إرسال تعليق