NA EMMANUEL MBATILO
KLABU ya Yanga imeendelea kuusogelea ubingwa wa Ligi ya NBC mara baada ya kufanikiwa kuichapa Singida Big Star kwa mabao 2-0, mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Liti mkoani Singida.
Yanga ilianza kupata bao la mapema kupitia kwa Aziz Ki huku bao la pili likifungwa na Clement Mzize na kuisadia timu yao kuongoza katika kipindi cha kwanza kwa mbao 2-0.
Kipindi cha pili Yanga ilirudi ikiwa inahitaji mabao zaidi kwani ilikuwa inalisakama lango la mpinzani japokuwa hawakufanikiwa kuongeza mabao mengine mpaka dakika 90 mpira kumalizika matokeo yakiwa 2-0.
Yanga Sc sasa inaendelea kukaa kileleni mwa ligi ikiwa na pointi 71 wakiwa wameshuka dimbani mara 27 huku nafasi ya pili akiwa bado inashikwa na timu ya Simba ambao hapo jana walialzimishwa sare na Namungo Fc na kuwafanya wapinzani wao Yanga kukaribia ubingwa wa ligi hiyo.
إرسال تعليق