BARABARA ZA LAMI KM 535 KUJENGWA KWA MARADI WA RISE


OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Angellah Kairuki amesema mradi wa uboreshaji wa barabara za vijijini kwa ushirikishaji na ufunguaji wa fursa za kijamii na kiuchumi (RISE) unaotekelezwa chini ya TARURA utajenga barabara Km 535 katika mikoa 4 ya nchini.



Mhe. Kairuki ameyasema hayo wakati wa hafla ya utiaji saini  Mikataba ya Ujenzi wa barabara za Mtili - Ifwagi (Km 14) na Wenda - Mgama (Km 19) mkoani Iringa kwa kiwango cha Lami iliyofanyika kwenye Manispaa ya Iringa tarehe 20.06.2023



Amesema mradi huu umeanza Nov.2021 na utakamilika June,2027 utahusisha ujenzi wa barabara za Mikoa Km 135 zilizoko chini ya TANROAD, ujenzi wa barabara za Wilaya Km 400 za TARURA, Matengenezo ya Maeneo korofi  km 4,500 -TARURA, Matengenezo ya kawaida ya Barabara kwa kutumia vikundi km 23,000- TARURA pia kupitia mradi huu ajira 35,000 zinatarajiwa kupatikana.

Mhe. Kairuki amebainishea uboreshaaji wa barabara za vijijini kupitia mradi huu ni dhahiri kuwa utachangia katika kupunguza umaskini kwenye maeneo yatakayopitiwa na mradi, utawezesha ufikaji kwenye maeneo ya uzalishaji (Mashambani, maghala na masoko ya mazao) na pia utakuza kilimo na kufugua fursa mbalimbali za kiuchumi ambapo jamii husika itashirikishwa.

Mradi unatarajiwa pia kushirikisha jamii katika kazi za Ujenzi wa Barabara hususani matengenezo ya kawaida (routine maintenance) kwa kutumia vikundi vinavyoundwa na watu wanaoishi katika maeneo ya Jirani na barabara pamoja na kuandaa mfumo wa kutumia takwimu kwa ajili kutoa vipaumbele kwenye ujenzi wa barabara za vijijni nchini amesisitiza.

Aidha Mhe. Kairuki amewaagiza Watendaji wa TARURA kuhakikishs  wanasimamia kwa karibu Wakandarasi na  ili mradi ukamilike kwa wakati na kwa ubora uliokusudiwa na
 fidia kwa waathirika wa miradi inayofuata zifanyika mapema kama ilivyofanyika kwa mradi huu, ili kuepusha ucheleweshaji wa mradi.

Pia amesisitiza utaratibu wa kutumia vikundi katika matengenezo ya barabara unakuwa endelevu. Utaratibu huu uzingatie makundi mbalimbali (Vijana, wazee na watu wenye ulemamvu


Maeneo yatakayopitiwa na mradi huu ni Wilaya ya Iringa, Kilolo na Mfundi (Iringa), Wilaya ya Handeni (Tanga)  Wilaya ya Mbogwe (Geita) pamoja na Wilaya ya Ruangwa iliyoko mkoani Lindi.

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA