Ofisa Rasilimali Watu wa Barrick North Mara ,Gloria Jimmy akizungumza katika kongamano la kuwajengea uwezo wanafunzi wa Vyuo vikuu vilivyopo mikoa ya Arusha na Kilimanjaro lililoandaliwa na taasisi ya AIESEC Tanzania na kufanyika katika Chuo cha Uhasibu Arusha(IAA), jijini Arusha kwa udhamini wa kampuni ya Barrick.Wengine pichani ni wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Graduate accountant kutoka kampuni ya Barrick,Solomon David, akizungumza na wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya mikoa ya Arusha na Kilimanjaro,katika kongamano lililoandaliwa na taasisi ya AIESEC Tanzania na kufanyika katika Chuo cha Uhasibu Arusha(IAA),jijini Arusha kwa udhamini wa kampuni ya Barrick.Wengine pichani ni wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Msimamizi wa mafunzo kutoka mgodi wa Barrick Bulyanhulu wa ,Masongo Masath,akizungumza katika kongamano hilo
Afisa Rasilimali Watu wa mgodi wa Barrick North Mara, Renus Mtafembwa,akizungumza na wanafunzi wa vyuo mbalimbali vya mikoa ya Arusha na Kilimanjaro,katika kongamano lililoandaliwa na taasisi ya AIESEC Tanzania na kufanyika katika Chuo cha Uhasibu Arusha(IAA),jijini kwa udhamini wa kampuni ya Barrick
Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria kongamano hilo wakifuatilia mada za kuwajengea uwezo kutoka kwa wataalamu mbalimbali.
Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria kongamano hilo wakifuatilia mada za kuwajengea uwezo kutoka kwa wataalamu mbalimbali.
Maofisa wa Barrick walipata fursa ya kutembelea maonyesho ya wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali.
Baadhi ya wadau kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo Kampuni ya uchimbaji madini ya Barrikck,wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa kongamano lililoshirikisha wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali vilivyopo mkoa wa Arusha na Kilimanjaro, lililoandaliwa na Taasisi ya AISEC Tanzania chini ya udhamini mkuu wa Kampuni ya Barrick,jana jijini Arusha katika Chuo cha Uhasibu Arusha(IAA).
****
Kampuni ya Barrick Gold Corporation, imedhamini na kushiriki katika kongamano la wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyopo katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro lililoandaliwa na taasisi ya kuchipua na kuendeleza vipaji vya uongozi kwa vijana (AIESEC Tanzania) lililofanyika katika Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) na kuwashirikisha wanafunzi,wahadhiri na wadau mbalimbali.
Kupitia kongamano hili ambalo hufanyika kila mwaka, wanafunzi huweza kufahamu jinsi taasisi mbalimbali nchini zinavyoendesha shughuli zake lengo kubwa ikiwa ni kuwajengea uwezo wa kujua vipaji walivyonavyo, kujifunza jinsi ya kujiamini na kukabiliana na ushindani katika soko la ajira, kujitambua uwezo wao ni jinsi gani wanaweza kushiriki kutoa mchango wa kuendeleza taifa pindi wamalizapo masomo yao.
Maofisa Raslimali Watu Waandamizi wa Barrick pia walishiriki katika maonesho na kongamano hilo ambapo walipata fursa kuzungumza na wanafunzi kuhusiana na kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ajira,kuendeleza vipaji vyao pia wanafunzi walipata fursa kuelewa jinsi kampuni ya kimataifa ya Barrick, inavyoendesha shuguli zake kwa kutoa kipaumbele kusaidia jamii sambamba na mpango wake wa kuibua na ukuzaji wa vipaji kwa vijana wa kitanzania na wafanyakazi wake.
إرسال تعليق