Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog
Uongozi wa Chemba ya Biashara ,Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoa wa Shinyanga umekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme kujadili mambo mbalimbali kuhusu sekta ya viwanda na ujasiriamali.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo Jumatatu Juni, 26 2023, kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga yenye lengo la kujadili kwa pamoja masuala ya uwekezaji katika viwanda, biashara na kilimo kwenye mkoa huo.
Akizungumza wakati wa kikao hicho kifupi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme amusihi uongozi wa TCCIA kufanya uhamasishaji kwa wadau mbalimbali kuwekeza mkoani humo hususani kwenye sekta yabiashara na viwanda.
“Sekta binafsi ina mchango mkubwa katika maendeleo kwa kutoa ajira kwa vijana na kuongeza pato la kiuchumi, kwa kutambua mchango huo serikali itaendelea kuunga mkono jitihada hizo na mimi kama katibu wa baraza la biashara mkoa niwaahidi ushirikiano wakati wote, na niwasihi tuendelee kuhamasisha wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali kuja kuwekeza kwenye mkoa wetu kupitia kilimo, biashara na viwanda kwani bado tuna maeneo makubwa kwaajili ya uwekezaji”, amesema RC Mndeme.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Shinyanga Jonathan Manyama ameushukuru uongozi wa mkoa kwa kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa wawekezaji na kuahidi kuendelea kushirikiana katika kuimalisha uchumi wa mkoa huo.
Katika hatua nyingine uongozi wa TCCIA Mkoa wa Shinyanga umefanya kikao cha ndani kilichoambatana na makabidhiano ya ofisi baina ya aliyekuwa Mwenyekiti wa TCCIA Dkt. Meshack Kulwa na Mwenyekiti mpya Jonathan Manyama yaliyofanyika katika ofisi za TCCIA Mkoa wa Shinyanga zilizopo Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati alipokutana na Uongozi wa TCCIA Mkoa wa Shinyanga ofisini kwake.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati alipokutana na Uongozi wa TCCIA Mkoa wa Shinyanga ofisini kwake.
Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Shinyanga Jonathan Manyama akikabidhi kitabu chenye muongozo na katiba ya TCCIA kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme.
Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo TCCIA Mkoa wa Shinyanga Jonathan Manyama akizungumza wakati wa kikao na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Makamu Mwenyekiti TCCIA Mkoa wa Shinyanga Hatibu Mgeja akizungumza wakati wa kikao na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Katibu wa TCCIA Mkoa wa Shinyanga Marcelina Saulo Akizungumza wakati wa kikao na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
Viongozi wa TCCIA Mkoa wakizungumza kabla ya kukutana na Mkuu wa Mkoa Shinyanga.
Mwenyekiti TCCIA Jonathan Manyama akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Shinyanga Hatibu Mgeja
Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Shinyanga Kulia akiwa na Makamu Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Shinyanga Hatibu Mgeja.
Katibu wa TCCIA Mkoa wa Shinyanga Marcelina Saulo akisikiliza wakati wa kikao cha makabidhiano.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Shinyanga Dkt. Meshack Kulwa.
Mwenyekiti mpya wa TCCIA Mkoa wa Shinyanga Jonathan Manyama akizungumza wakati wakati wa kikao cha makabidhiano ya ofisi.
Picha ya pamoja ya Uongozi wa TCCIA Mkoa wa Shinyanga.
إرسال تعليق