UWT SHINYANGA MJINI WACHANGAMKIA AKAUNTI YA MWANAMKE HODARI BENKI YA AZANIA

Zoezi la kujisajili na Akaunti ya Mwanamke Hodari likiendelea
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini, Rehema Nhamanilo akijisajili na Akaunti ya Mwanamke Hodari

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Wajumbe wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Wilaya ya Shinyanga Mjini wamechangamkia fursa ya Akaunti ya Mwanamke Hodari inayopatikana katika Benki ya Azania ambayo walengwa ni Wanawake wajasiriamali, vikundi vya wanawake vya kijasiriamali, kampuni zenye umiliki mkubwa wa wanawake na kampuni zenye waajiriwa wengi wanawake.

Wanawake hao wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini wamejisajili bure katika Benki ya Azania na kupatiwa bure kadi ya Visa (ATM) Jumamosi Julai 8,2023 kwenye Baraza la UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini wakati Maafisa wa Benki ya Azania wakitoa elimu kuhusu huduma zinazotolewa katika Benki hiyo ikiwemo Akaunti na Mikopo maalumu kwa ajili ya wanawake (Akaunti ya Mwanamke Hodari).

Akielezea kuhusu Akaunti Mwanamke Hodari, Afisa Uhusiano Benki ya Azania tawi la Kahama Bi. Dorah Chacha  amesema Akaunti ya Mwanamke Hodari inafunguliwa bure bila kiwango cha kuanzia, kutoa hela dirishani bure, hakuna makato ya mwezi  na unapata kadi ya Visa (ATM) inayokuwezesha kuchukua pesa katika Benki yoyote.
Afisa Uhusiano Benki ya Azania tawi la Kahama Bi. Dorah Chacha

“Sifa za Mikopo ya Hodari ni kwamba  ina Riba nafuu ya 1% tu kwa mwezi, Mkopo kuanzia Sh.200,000 mpaka milioni 500, ukiwa na akaunti ya Mwanamke hodari utaweza kukopa mara nne (4) ya akiba aliyoweka Benk na Mikopo ni kwa vikundi na mfanyabiashara mmoja mmoja”,amesema Dorah.

Amefafanua kuwa Mwanamke Hodari ni yule anayetimiza malengo kwa juhudi na mikakati maalum, mwanamke asiyekata tamaa, hufanya lolote zuri na lenye faida kutimiza malengo yake kibiashara ili kupata riziki.

“Benki ya Azania inaungana nawe mwanamke hodari kwa kukutengenezea akaunti na mikopo sahihi kwa ajili yako wewe ambaye ni mwanamke wa kisasa, jasiri, imara unayejali maendeleo na mwenye maono ya kusimamia yale yanayonufaisha maisha yako na jamii inayokuzunguka. Karibuni sana Wanawake wajasiriamali, vikundi vya wanawake vya kijasiriamali, kampuni zenye umiiki mkubwa wa wanawake na kampuni zenye waajiriwa wengi wanawake”,amesema Dorah.
Afisa Uhusiano Benki ya Azania tawi la Kahama Bi. Dorah Chacha akielezea kuhusu Akaunti ya Mwanamke Hodari kwa wajumbe wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini . Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa Uhusiano Benki ya Azania tawi la Kahama Bi. Dorah Chacha akielezea kuhusu Akaunti ya Mwanamke Hodari kwa wajumbe wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini 

Maafisa wa Benki ya Azania wakigawa vipeperushi vinavyoelezea Akaunti ya Mwanamke Hodari kwa wajumbe wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini 
Mjumbe wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini akisoma kipeperushi kinavyoelezea Akaunti ya Mwanamke Hodari 
Afisa wa Benki ya Azania akijaza taarifa za Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini, Sharifa Hassan Mdee (kulia) wakati akijisali na Akaunti ya Mwanamke Hodari
Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini, Sharifa Hassan Mdee (kulia)  akijisajili na Akaunti ya Mwanamke Hodari

Maafisa wa Benki ya Azania na viongozi wa UWT wakiwa kwenye kikao cha UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini
Maafisa wa Benki ya Azania wakiwa kwenye kikao cha UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA