MKUU WA MKOA WA MBEYA AZINDUA MABASI YA KISASA ACHIMWENE SAFARI


Na mwandishi wetu Mbeya

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Juma Zuberi Homera amezindua mabasi mapya ya kisasa Achimwene safari.

Mhe.Homera ameipongeza sana kampuni ya Achimwene safari kwa kuendelea kufanya uwekezaji huu mkubwa ndani ya Mbeya na Tanzania  kwa sababu wanaendelea kumuunga mkono Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kukuza uchumi wa Nchi.


Mhe. Homera amezindua mabasi hayo leo Agosti 12,2023 akimpongeza sana mkurugenzi wa kampuni hiyo Bwana Heneriko Achimwene kwa uzalendo huu mkubwa, vijana wanapata ajira.

Mhe.Homera amesema serikali ya Mkoa wa Mbeya itaendelea kuunga mkono jitihada za kampuni ya Achimwene waendelee kuwekeza zaidi na zaidi.

Pia amewaomba wana Mbeya na watanzania kumuunga Mkono mwekezaji huyu ili aendelee kuwekeza zaidi na zaidi kwa maana mabasi haya ni ya kisasa yana choo ndani yataepusha ajari na kupunguza usumbufu wa kushuka shuka kuchimba dawa.


Aidha ametoa rai kwa madereva wote Tanzania kuendesha mabasi kwa kufuata sheria za barabarani kuepusha ajali zisizo za lazima, kwa wasiofuata sheria hizo na kusababisha ajali watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Naye mkurugenzi wa kampuni ya Achimwene Bwana Heneriko Achimwene ameishukuru sana serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ushirikiano mkubwa hali inayosababisha mpaka vijana wanaendelea kufanya uwekezaji kama huo.


Pia mtendaji mkuu Bwana Innocent Joseph amewashukuru  watanzania wote kwa kuendelea kushirikiana na kampuni ya Achimwene akisema mabasi haya ni ya watanzania, safari zake ni kutoka Mbeya kwenda Dar es salaam na kutoka Dar es salaam kwenda Mbeya kila siku.


Katika hafla hiyo ya uzinduzi wa mabasi hayO mapya Achimwene safari wadau mbalimbali walihudhuria akiwemo msanii wa kuigiza sauti za viongozi Oscar Nyerere kama balozi wa mabasi hayo.
Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA