Meneja Miradi wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited Angelina Lameck Magoti akifungua bomba la maji katika Mradi Mpya wa Uuzaji wa Viwanja vya Makazi na Biashara uitwao Oysterbay Project katika eneo la Mwalugoye kata ya Chibe katika Manispaa ya Shinyanga ambapo kila kiwanja kimesogezewa maji
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited imetambulisha na kuzindua Mradi Mpya wa Uuzaji wa Viwanja vya Makazi na Biashara uitwao Oysterbay Project katika eneo la Mwalugoye kata ya Chibe katika Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika leo Jumamosi Septemba 23,2023 Mkurugenzi wa Miradi na Uwekezaji wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Japhet Allex Bulugu amesema Mradi wote umeshawekewa barabara pamoja na beacons na kila kiwanja kimesogezewa maji.
Ameeleza kuwa huduma za kibinadamu kama umeme, shule, zahanati na eneo la kuchezea watoto na vingine vingi, vyote vinapatikana katika mradi huo mpya.
“Mradi huu ni wa kishua kweli kweli upo kilomita 4 tu kutoka katikati ya Manispaa ya Shinyanga. Eneo hili lipo barabarani kabisa kwenye lami uelekeo wa Old-Shinyanga palipo na kona ya Chibe. Kitu cha kipekee sana ni kwamba tumesogeza maji kwenye kila kiwanja ambapo maji yapo mita 5 kwa kila kiwanja, mradi upo jirani na makazi ya watu. Hapa pia tumeweka eneo la wazi kwa ajili ya kuchezea watoto”,amesema Bulugu.
Amesema Viwanja hivyo vimepimwa kulingana na viwango vinavyotakiwa na Wizara ya Ardhi ili kuondoa makazi holela.
"Ishi Kijanja, ishi kishua kwa kujipatia Kiwanja/ Plot moja kuanzia Tsh 7,000/= (plot za makazi) na 7,500/=(plot za makazi na biashara) kwa square meter moja. Ukikamilisha malipo unapata mkataba wa mauziano na hati ya kiwanja yenye jina lako bure kabisa”,ameeleza Bulugu
Amefafanua kuwa, malipo ni Cash na Installment, ukilipa cash unapata punguzo la Tsh 300/= kwa kila square meter ambapo Installment (kidogokidogo) ni awamu tatu tu, utatanguliza asilimia 50 yaani nusu ya gharama, kisha utalipa robo ya kwanza na robo ya pili(1/2,1/4,1/4).
“Kwenda Site ni bure na ukiwa mbali tutakutumia ramani uchague huko huko. Wasiliana nasi sasa kwa simu 0677000026/0677000028 au fika ofisini kwetu Shinyanga Jengo la NSSSF Mpya - Barabara kuu ya Mwanza Ghorofa Na 1. Kumbuka, Ujanja ni Kiwanja na viwanja ni Oysterbay”,amesema Bulugu.
Mkurugenzi wa Fedha Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Peter Joseph Charles amezitaja huduma wanazotoa katika Kampuni hiyo kuwa pamoja na Uendelezaji wa ardhi, ushauri kuhusu masuala ya ardhi, usimamizi wa mali yakiwemo majengo, magari na viwanja, ukusanyaji wa ushuru na mikopo, udalali, uchoraji wa ramani za majengo, uuzaji wa vifaa vya ujenzi pamoja na kufanya tafiti mbalimbali.
Amesema tangu kuanzishwa kwa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited mwaka 2021 wamekuwa na mafanikio makubwa ya kuuza viwanja vyote kwani wananchi wameendelea kuwa na imani na Kampuni hiyo yenye makao makuu yake Mjini Shinyanga.
"Miongoni mwa miradi yetu ambayo tumeifanya ni pamoja na mradi wa Diamond City 1 & 2 ipo Ibadakuli karibu na Savanna Plains, SGR VIEW Project upo Mwalugoye karibu na Stesheni ya SGR, Brotherhood Village 1 & 2 upo Mwalugoye Jirani na Hilbart English Medium Oysterbay Project katika eneo la Mwalugoye kata ya Chibe katika Manispaa ya Shinyanga",amesema Charles.
Mkurugenzi wa Miradi na Uwekezaji wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Japhet Allex Bulugu akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi Mpya wa Uuzaji wa Viwanja vya Makazi na Biashara uitwao Oysterbay Project katika eneo la Mwalugoye kata ya Chibe katika Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Septemba 23,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Miradi na Uwekezaji wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Japhet Allex Bulugu akielezea kuhusu Mradi Mpya wa Uuzaji wa Viwanja vya Makazi na Biashara uitwao Oysterbay Project katika eneo la Mwalugoye kata ya Chibe katika Manispaa ya Shinyanga

Mkurugenzi wa Fedha Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Peter Joseph Charles akielezea kuhusu Kampuni hiyo na Mradi Mpya wa Uuzaji wa Viwanja vya Makazi na Biashara uitwao Oysterbay Project katika eneo la Mwalugoye kata ya Chibe katika Manispaa ya Shinyanga

Keki maalumu wakati wa uzinduzi wa Mradi Mpya wa Uuzaji wa Viwanja vya Makazi na Biashara uitwao Oysterbay Project katika eneo la Mwalugoye kata ya Chibe katika Manispaa ya Shinyanga
Zoezi la kukata Keki maalumu wakati wa uzinduzi wa Mradi Mpya wa Uuzaji wa Viwanja vya Makazi na Biashara uitwao Oysterbay Project katika eneo la Mwalugoye kata ya Chibe katika Manispaa ya Shinyanga
Zoezi la kukata Keki maalumu wakati wa uzinduzi wa Mradi Mpya wa Uuzaji wa Viwanja vya Makazi na Biashara uitwao Oysterbay Project katika eneo la Mwalugoye kata ya Chibe katika Manispaa ya Shinyanga
Meneja Miradi wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited Angelina Lameck Magoti akimlisha keki Mkurugenzi wa Miradi na Uwekezaji wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Japhet Allex Bulugu wakati wa uzinduzi wa Mradi Mpya wa Uuzaji wa Viwanja vya Makazi na Biashara uitwao Oysterbay Project katika eneo la Mwalugoye kata ya Chibe katika Manispaa ya Shinyanga
Meneja Miradi wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited Angelina Lameck Magoti akimlisha keki Mkurugenzi wa Fedha Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Peter Joseph Charles wakati wa uzinduzi wa Mradi Mpya wa Uuzaji wa Viwanja vya Makazi na Biashara uitwao Oysterbay Project katika eneo la Mwalugoye kata ya Chibe katika Manispaa ya Shinyanga
Zoezi la kulishana keki likiendelea wakati wa uzinduzi wa Mradi Mpya wa Uuzaji wa Viwanja vya Makazi na Biashara uitwao Oysterbay Project katika eneo la Mwalugoye kata ya Chibe katika Manispaa ya Shinyanga

Wafanyakazi wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited wakiendelea kufanya kazi katika Mradi Mpya wa Uuzaji wa Viwanja vya Makazi na Biashara uitwao Oysterbay Project katika eneo la Mwalugoye kata ya Chibe katika Manispaa ya Shinyanga
Meneja Miradi wa Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited Angelina Lameck Magoti kifungua bomba la maji katika Mradi Mpya wa Uuzaji wa Viwanja vya Makazi na Biashara uitwao Oysterbay Project katika eneo la Mwalugoye kata ya Chibe katika Manispaa ya Shinyanga ambapo kila kiwanja kimesogezewa maji
Mkurugenzi wa Fedha Kampuni ya Brotherhood Survey Services Company Limited, Peter Joseph Charles akionesha miundombinu ya umeme iliyopo jirani na Mradi Mpya wa Uuzaji wa Viwanja vya Makazi na Biashara uitwao Oysterbay Project katika eneo la Mwalugoye kata ya Chibe katika Manispaa ya Shinyanga
Wadau wakiangalia viwanja katika Mradi Mpya wa Uuzaji wa Viwanja vya Makazi na Biashara uitwao Oysterbay Project katika eneo la Mwalugoye kata ya Chibe katika Manispaa ya Shinyanga.
Mdau akioneshwa ramani ya viwanja katika Mradi Mpya wa Uuzaji wa Viwanja vya Makazi na Biashara uitwao Oysterbay Project katika eneo la Mwalugoye kata ya Chibe katika Manispaa ya Shinyanga.
Wadau wakiangalia viwanja katika Mradi Mpya wa Uuzaji wa Viwanja vya Makazi na Biashara uitwao Oysterbay Project katika eneo la Mwalugoye kata ya Chibe katika Manispaa ya Shinyanga.
Sehemu ya eneo la Mradi Mpya wa Uuzaji wa Viwanja vya Makazi na Biashara uitwao Oysterbay Project katika eneo la Mwalugoye kata ya Chibe katika Manispaa ya Shinyanga.
Sehemu ya eneo la Mradi Mpya wa Uuzaji wa Viwanja vya Makazi na Biashara uitwao Oysterbay Project katika eneo la Mwalugoye kata ya Chibe katika Manispaa ya Shinyanga.
إرسال تعليق