DKT. BITEKO AIAGIZA WIZARA YA ARDHI KUPANGA, KUPIMA NA KUMILIKISHA ARDHI KWA UFANISI

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Dkt. Doto Biteko (kushoto) akikabidhiwa moja ya vifaa vitakavyotumika katika shughuli za upimaji ardhi nchini, anayemkabidhi ni Balozi wa Korea Kusini nchini, Kim Su Pyo.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Dkt. Doto Biteko (kulia) akimkabidhi moja ya vifaa vitakavyotumika katika shughuli za upimaji ardhi nchini, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Jerry Silaa.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Dkt. Doto Biteko (kulia) akimkabidhi cheti mmoja wa wakufunzi Kumi  waliopata mafunzo ya kurusha ndege zisizo na rubani zitakazotumika katika shughuli za upimaji ardhi nchini.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Dkt. Doto Biteko akizungumza  wakati wa hafla ya kuzindua kituo cha Taifa cha Ubunifu na Mafunzo ya taarifa  za kijiografia kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe.Kassim Majaliwa.

✔️Atoa angalizo la kutogeuka kuwa Wizara ya kutatua migogoro ya ardhi
 ***
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Doto Biteko ameiagiza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kufanyia kwa ufanisi majukumu yake ya msingi ambayo ni kupanga, kupima na kumilikisha ardhi ili kuondoa migogoro ya ardhi inayotokea nchini na kuifanya Wizara husika kuishughulikia mara kwa mara.

Ameyasema hayo tarehe 9 Septemba, 2023 jijini Dodoma wakati wa hafla ya kuzindua kituo cha Taifa cha Ubunifu na Mafunzo ya taarifa za kijiografia kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe.Kassim Majaliwa.

“ Kazi za Wizara hii ni tatu, ambazo  ni kupanga, kupima na kumilikisha ardhi, sasa tujipime na tujitathmini kama katika sekta yetu ya ardhi kazi hizi tunazifanya kwa ukamilifu wake, lipo wimbi la kuweka tension ya Wizara kutoka kwenye Sheria yake au Ilani ya uchaguzi na kugeuka kuwa Wizara ya utatuzi wa migogoro ya ardhi; kuanzia sasa tuwafanye  watanzania wazungumze mipango miji, maendeleo ya makazi na matumizi bora ya ardhi.” Amesisitiza Dkt. Biteko

Ameitaka Wizara hiyo pia kushirikiana na Halmashauri zote nchini ili kazi zifanyike kwa ufanano na hivyo kwa pamoja waweze kuondoa urasimu na  kuondoa migogoro ya ardhi na  hivyo ana imani kuwa Wizara hiyo itamaliza changamoto zilizopo na kuweza kupanga miji ipasavyo na kuimarisha makazi ya watu ili kujenga Tanzania iliyo bora zaidi.

“Wizara hii ni moyo wa shughuli za uchumi hapa nchini, kwani watu wanaofanya shughuli za ujenzi, kilimo, wanaojenga miradi mbalimbali ikiwemo ya gesi asilia, wanategemea Sekta ya Ardhi, pamoja na kazi kubwa iliyofanyika ya kuimarisha sekta hii bado kuna kazi kubwa mbele ya kujiimarisha.”Amesema Dkt. Biteko

Kuhusu kituo hicho alichokizindua, Dkt.Biteko amesema kuwa, ni muendelezo wa hatua zinazochukuliwa na Rais, Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuchochea matumizi ya teknolojia katika kuleta maendeleo endelevu na ubunifu hapa nchini.

Amesema kuwa kituo hicho ni muhimu kwani kitaboresha shughuli za upimaji ardhi, uandaaji wa ramani za msingi, ujenzi wa miundombinu, kupanga matumizi bora ardhi pamoja na masuala mengine yanayohusiana na Sekta ya Ardhi. Ametoa wito kwa Wizara na Taasisi zake kupeleka watumishi kwenye kituo hicho ili wapate mafunzo ya ukusanyaji, uchakataji na utumiaji wa taarifa za kijiografia katika kutekeleza majukumu ya taasisi zao.

Ametoa pongezi kwa Chuo Kikuu cha Dodoma kwa kutoa eneo na jengo kwa ajili ya kuanzisha kituo hicho, pia ameishukuru Serikali ya Korea Kusini kwa kugharamia uanzishaji wa kituo hicho.

Aidha, amewataka wahitimu kutoka Kituo hicho wakafundishe watumishi wengine na wakawe chachu ya mabadiliko ya kiutendaji katika Sekta na kuongeza matumizi ya taarifa za kijiografia nchini.

Hafla hiyo ya uzinduzi wa kituo cha Taifa cha Ubunifu na Mafunzo ya taarifa za kijiografia ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Caption
Moja


Mbili


Mbili


Tatu

Nne 

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA