USIKU WA WADAU WA HABARI NA VYOMBO VYA HABARI KANDA YA ZIWA KUFANYIKA SEPTEMBA 29

 


Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (Mwanza Press Club - MPC) imeandaa Usiku wa marafiki na wadau wa vyombo vya habari Kanda ya Ziwa, unaotaraji kufanyika Septemba 29, 2023.

Lengo kuu ni kuwapa nafasi wadau wa vyombo vya habari kueleza utekelezaji wa mipango yao kwa mwaka 2023 mbele ya vyombo vya habari.

Pia malengo madogo ni, kuwapa nafasi wadau wa habari kutangaza huduma na bidhaa wanazozalisha/ kutoa, kuwapa nafasi wananchi kuzijua taasisi za umma na binafsi na kazi wanazozifanya na pia kujenga mahusiano ya kiutendaji baina ya serikali, taasisi za kiserikali, AZAKI na mashirika binafsi na vyombo vya habari.


Faida za kushiriki ni wadau watapata nafasi ya kushiriki wiki ya wadau wa habari kabla ya usiku wa wadau wa habari, ambapo waandishi wa habari watatembelea taasisi zitakazoshiriki, logo za wadau zitachapishwa kwenye tshirt na mabango yote, kila mdau atapata nafasi ya kunadi taasisi yake.

Mratibu MPC
6.8.2023
Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA