MCHENGERWA AIELEKEZA TARURA KUKUZA KAMPUNI ZA WAKANDARASI WAZAWA

 Na, Nteghenjwa Hosseah - TAMISEMI
 
WAZIRI wa Nchi,  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa ametangaza rasmi mkakati wa kukuza na kuendeleza wakandarasi wazawa ili wafikie viwango vya kimataifa vya ubora na usalama.

Mchengerwa ameyasema hayo leo wakati wa kikao na watumishi wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kilichofanyika Makao Makuu ya TARURA Jijini Dodoma.

Amesema Serikali imejipanga vyema kuhakikisha inawanyanyua wakandarasi wazawa na kusisitiza kuwa pamoja na majukumu ya TATURA pia  wanalo jukumu la kukuza na kuwaendeleza wakandarasi wazawa.

"Hatuwezi kuitenganisha TARURA na wakandarasi wa ndani kama ambavyo huwezi kuitenganisha TAMISEMI na wananchi, maendeleo ya miundombinu yanamchango katika uchumi wa wananchi na wa Taifa."

"Mikakati ya TARURA ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2025 tuwe tumeboresha barabara za vijijini na mijini kwa asilimia 85 lakini tukiwa tunaenda kuyafikia mafanikio hayo lazima tujiulize tumewakuza na kuwajenga wakandarasi wangapi wazawa?

tumewanyanyua kiasi gani kufikia viwango vya kuwafanya washindane kimataifa."
" Kwa hiyo ninawataka, pamoja na majukumu mengi mliyonayo TARURA kwenye uongozi wangu kama Waziri jukumu la kukuza na kuwaendeleza wakandarasi wazawa nitalipa kipaumbele cha hali ya juu. Na leo natangaza rasmi mkakati wa kukuza wakndarasi wazawa utakaosimamiwa na ninyi TARURA."

" Nitawapa TARURA mnisaidie ili tunakokwenda tuwe tumewajenga wakandarasi  alteast kila mkoa  kampuni za wakandarasi 20 tutakua kumekuza Kampuni za Wakandarasi takribani 520 katika mikoa yetu yote 26."

"Tukiyashika mkono kampuni ya wazawa wa kitanzania  20 kila mkoa ina maana tutafungua uchumi na kustawi kwa kila mkoa, pia itawezesha kuimalisha kazi za wakandarasi hao kwa kila mkoa."

Alisema mpango mkakati huo ni wa kuziwezesha kampuni za wazawa za ujenzi ili ziweze kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa miradi inayotangazwa na TARURA.

"Lengo kuu la mpango huu ni kuboresha mazingira ambayo mjasiliamali wa Kitanzania wanaweza kufaulu, kukua na kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi."

Alisema pia umelenga kujenga Tanzania yenye nguvu inayojitegemea na ambayo inaweza kukabiliana na changamoto za karne ya 21 kwa kutumia uwezo wa wakandarasi wa ndani.

Mchengerwa pia ameiangiza TARURA kuandaa utaratibu wa wazi wa namna ya kuwachangua kampuni hizo 20 kwa kila mkoa na kusisitiza kuwa mchakato wa haki.
 
Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA