RAIS SAMIA APEWA TUZO YA NAMBA 1 SHINYANGA

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi  (kushoto) aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la kumpongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme Tuzo ya Heshima na Pongezi yenye alama ya Namba 1 kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyotolewa na Wanawake wa Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Oktoba 30,2023. 

Na Kadama Malunde- Malunde 1 blog

Wanawake Mkoa wa Shinyanga wametoa Tuzo ya Heshima na Pongezi yenye alama ya Namba 1 kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kuleta maendeleo katika mkoa wa Shinyanga na Tanzania kwa ujumla ambapo kila kijiji kimefikiwa.

Tuzo hiyo imekabidhiwa leo Jumatatu Oktoba 30,2023 na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi kwa Mkuu wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme aliyeipokea kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akikabidhi tuzo hiyo, Mhe. Samizi ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la kumpongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za kutekeleza miradi mingi ya maendeleo katika sekta zote ikiwemo afya, elimu maji na nishati ya umeme lililofanyika Oktoba ,12,2023 katika Manispaa ya Shinyanga likiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amesema tuzo hiyo ni mwendelezo wa Kongamano hilo.

“Katika Kongamano la kumpongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, tuliahidi kuwa tutatoa zawadi kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na maendeleo aliyoyaleta Mkoani Shinyanga. Tumempa tuzo ya shukrani na pongezi kwa sababu amegusa vijiji vyote, vijiji vyote vimefikiwa kutokana na mvua ya mabilioni ya fedha yanayotolewa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kutekeleza miradi ya maendeleo”,amesema Mhe. Samizi.

Akipokea tuzo hiyo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amewashukuru wanawake wa mkoa wa Shinyanga kwa kutambua kazi kubwa inayofanywa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuwaletea maendeleo wananchi wa mkoa wa Shinyanga.

“Naipongeza sana Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la Kumpongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan,ninakiri kupokea tuzo hii yenye alama ya Namba moja (1) kutoka kwa wanawake wa mkoa wa Shinyanga na nitaifikisha kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan”,amesema Mndeme.

“Kwa niaba ya wanawake kutoka wilaya zote za Mkoa wa Shinyanga tunakupongeza Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kuleta maendeleo Mkoa wa Shinyanga na Tanzania kwa ujumla. Vijiji vyote vimefikiwa”,ameongeza Mndeme.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akionesha Tuzo ya Heshima na Pongezi yenye alama ya Namba 1 kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyotolewa na Wanawake wa Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Oktoba 30,2023. 

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza baada ya kukabidhiwa Tuzo ya Heshima na Pongezi yenye alama ya Namba 1 kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyotolewa na Wanawake wa Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Oktoba 30,2023.  

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi  (kushoto) ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la kumpongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan  akizungumza wakati akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme Tuzo ya Heshima na Pongezi yenye alama ya Namba 1 kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyotolewa na Wanawake wa Mkoa wa Shinyanga leo Jumatatu Oktoba 30,2023.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi  (kushoto) ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la kumpongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan  akizungumza wakati akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme Tuzo ya Heshima na Pongezi yenye alama ya Namba 1 kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyotolewa na Wanawake wa Mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akicheza na wanawake wakati wa akikabidhiwa Tuzo ya Heshima na Pongezi yenye alama ya Namba 1 kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyotolewa na Wanawake wa Mkoa wa Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiagana na wanawake wa mkoa wa Shinyanga baada ya kukabidhiwa Tuzo ya Heshima na Pongezi yenye alama ya Namba 1 kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyotolewa na Wanawake wa Mkoa wa Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA