SPIKA DKT. TULIA AZISAKA KURA ZA URAIS IPU ANGOLA

 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mgombea Urais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 23 Oktoba, 2023 ameshiriki vikao  vya  Makundi ya Mabara  yanayounda Umoja huo katika Ofisi za Bunge la Angola zilizopo Jijini Luanda kwa lengo la kujinadi na kueleza sababu za yeye kugombea nafasi hiyo.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Tulia amewaeleza Wajumbe wa Makundi hayo kuwa endapo watamchagua katika Uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Oktoba, 2023 atahakikisha anasimamia misingi ya Umoja huo kwa kuongeza Ufanisi, Uwajibikaji na Uwazi.













Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA