UZBEKISTAN
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Jasmine Kairuki (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Gavana wa jimbo la Kharezm, jijini Samarkand - Uzbekistan, Bw. Davletov Anvar Kenjayevich, kuhusu ushirikiano katika sekta ya utalii baina ya Tanzania na Uzbekistan leo Oktoba 15, 2023.
Waziri Kairuki pia atapata nafasi ya kutembelea Chuo Kikuu cha Utalii ili kuona uzoefu wa Uzbekistan katika mafunzo ya sekta ya utalii; na kutafuta nafasi za kujengewa uwezo kutoka kwao hasa ikizingatiwa kuwa jiji la Samarkand limeendelea kiutalii.
Vilevile, Mhe. Kairuki na ujumbe wake wanatarajia kuona uzoefu ilionao Uzbekistan katika uratibu wa makumbusho za Taifa.
إرسال تعليق