Na. Asila Twaha, Iringa
Timu ya wanawake ya kuvuta kamba na netiboli TAMISEMI zimeingia hatua ya mtoano baada ya kucheza mechi 4 na kushinda kupata nafasi nzuri kwa timu zote mbili kuingia hatua hiyo.
Mapema asubuhi Oktoba 3, 2023 katika viwanja vya Mkwawa Mkoani Iringa timu ya kamba ilicheza na wapinzani wake Wakili Mkuu na kuwashinda kwa pointi 2-0 huku timu ya netiboli kucheza katika uwanja wa Chuo Kikuu cha RUAHA kuwafunga wapinzani wao Ujenzi goli 29-21.
Kocha wa timu ya kamba TAMISEMI Chediel Masinga amesema pointi 7 walizoshinda kwa mechi nne walizocheza zimewapa nafasi kuingia katika hatua ya mtoano.
Amesema kwa hatua ya makundi timu ya TAMISEMI ilipangwa kundi F kucheza na RAS Kagera, Mashtaka, Mambo ya Nje na Wakili Mkuu na mechi zote hizo wamefanya vizuri.
Kwa upande wa timu ya netiboli kushinda na kufikia hatua ya mtoano walicheza na timu ya Mashtaka,TARURA,Ujenzi na Uchukuzi.
Michezo ya Shirikisho ya Wizara na Idara za Serikali yatafunguliwa tarehe 4 Oktoba, 2023.
Matukio Katika Picha Wakati wa Mchezo huo ukiendelea.
إرسال تعليق