Ukarabati wa Awamu ya Kwanza unaoendelea katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam umefikia asilimia 95 na asilimia tano zilizobaki zinatarajiwa kukamilika ndani ya siku tano kuanzia leo.
Akikagua ukarabati huo leo Oktoba 9, 2023, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro
amesema tayari vyumba vinne vya wachezaji, sehemu ya kuchezea, vyumba
vya waamuzi, afya na eneo la video za marejeo (VAR) umekamilika.
"
Tayari taa za kisasa 320 za mfumo wa LED zimefungwa na kuna huduma ya
mtandao wa bure kabisa kwa ajili ya watazamaji wa mechi ambao
tutauzindua kati ya tarehe 17 hadi 19 mwezi huu kabla ya mchezo wa
ufunguzi wa African Football League kati ya Timu ya Simba na Al Alhy ya
nchini Misri tarehe 20,2023 " amesema Mhe. Ndumbaro.
Ameongeza
kuwa, katika eneo la watu mashuhuri na sehemu ya wandishi wa Habari kazi
iliyobakia ni ndogo ambayo itamalizika ndani ya siku hizo tano
akiongeza kuwa mfumo wa sauti uwanjani tayari umerekebishwa.
Dkt.
Ndumbaro amesema kuwa Kampuni ya Formula 360, itafunga mfumo wa
matangazo kidijitali ambao utaanza kufanya kazi rasmi Oktoba 20, 2023
huku akisistiza kuwa baada ya mchezo huo, ukarabati mkubwa wa awamu ya
pili utaendelea.
إرسال تعليق