WATU 20 WAFARIKI DUNIA KWA AJALI - NZEGA MKOANI TABORA

 

Watu 20 wanahofiwa kufariki dunia baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugongana na lori mjini Nzega mkoani Tabora.

Akitoa taarifa ya ajali hiyo leo Jumamosi Oktoba 21, 2023, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Richard Abwao amesema ajali hiyo imehusisha basi la Alpha linalofanya safari zake kati Shinyanga na Dar es Salaam na kwamba wakati wa ajali, lilikuwa likitokea Shinyanga.
"Nimepata taarifa hiyo na sasa ndio naelekea eneo la tukio na taarifa kamili nitaitoa baada ya kufika na kujua hali ilivyo," amesema

Naye Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Naitapwaki Tukai amesema amepata taarifa ya ajali hiyo akiwa wilayani Sikonge katika maadhimisho ya miaka 100 ya Hospitali ya Misheni inayomilikiwa na Kanisa la Moravian, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk Batilda Burian.

Amesema baada ya baada ya kupata taarifa hiyo ameelekea kwenye eneo la tukio.

Hii ni ajali kubwa kuua idadi kubwa ya watu katika Mkoa wa Tabora kwa mwaka huu.

Soma hapa zaidi chanzo Mwananchi.
Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA