Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt Dotto Biteko amesema serikali imetoa BILIONI 170 kwa ajili ya utelekezaji wa miradi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) mkoani Mtwara.
Dkt Biteko ameiagiza REA kufanya tathimini ya wakandarasi wanaotekeza miradi ya umeme na kuachana na wale wanaoshindwa kuendana na kasi ili ifikapo Juni 2024, miradi yote nchini iwe imekamilika.
Naibu Waziri Mkuu ameipongeza REA kwa usimamizi mzuri wa miradi ya usambaji wa nishati vijijini ili kuhakikisha utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya upatikanaji wa nishati vijijini ifikapo 2025 inatimia.
Aidha, Dkt Biteko ameitaka REA na TANESCO kutumia vifaa vya usambazaji umeme vinavyozalishwa na viwanda vya ndani badala ya kuagiza nje ya nchi .
Naibu Waziri Mkuu ameyasema hayo tarehe 15 Novemba 2023 katika wilaya ya Mtwara mkoani Mtwara wakati akiwasha umeme katika vijiji vya Nachenjele na Naliendele katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
“REA msicheke na wakandarasi wanaokwamisha utelekezaji wa malengo yetu na hili linahitaji usimamizi wa karibu kwa kila miradi” amesema Dkt Biteko
Amesema wafanye tathimini ya wakandarasi na kuahidi kurudi baada ya miezi mitatu kuhakikisha wamekamilisha kama alivhoagiza.
“Tunataka tutoke kwenye miradi ya vijiji na tuingie katika kampeni ya kitongoji kwa kitongoji baada ya uchaguzi mkuu ujao” amesisitiza
Kwa upande wake Kaimu Mkurugezi Mkuu wa REA ambaye ni Mkurugenzi wa Umeme Vijijini, Mhandisi Jones Olotu amesema wamesambaza umeme katika vijiji 384 kati ya 785 ambapo vilivyosalia viko katika utekelezaji.
Amesema REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili unalenga kupeleka katika vijiji vyote 401 ambapo wakandarasi wanaendelea na kazi hizo.
Mhandisi Olotu amesema kuwa wanatekeleza miradi ya kusambaza umeme maeneo ya pembezoni mwa mji, mradi wa kupeleka umeme kwenye migodi midogo, maeneo ya kilimo, vituo vya afya na pampu za maji na miradi ya ujazilizi.
إرسال تعليق