Mbunge wa Jimbo la Lupembe Mkoa wa Njombe, Mhe. Edwin Enosy Swalle anawakaribisha Wananchi wote katika Mashindano ya Fainali ya Swalle CUP2023 itakayoambatana na na utoaji wa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mgeni rasmi katika mashindano ya Swalle CUP2023 anatarajiwa kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali ambapo mchezo utakuwa ni kati ya Igongo FC dhidi ya Matembwe FC hapo kesho.
Ikumbukwe kuwa Michezo katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, CCM 2020-2025 imepewa kipaumbele kikubwa kwani michezo ni ajira, michezo ni burudani, michezo ni afya na michezo inatuweka pamoja katika Umoja.
إرسال تعليق