Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege Hamis Kisesa aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza S. Johari akizungumza na wataalam wa Chama cha Waongozaji ndege Tanzania (TATCA) kuhusu namna Mamlaka ilivyojipanga kuwawezesha Waongozaji ndege kufanya kazi kwa weledi na ufanisi wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 43 wa mwaka uliofanyika Novemba 24, 2023 katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege Bw. Hamis Kisesa aliyemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza S. Johari amefungua mkutano wa 43 wa mwaka wa Chama cha Waongozaji Ndege Tanzania (TATCA) unaofanyika Peacock Hotel jijini Dar es Salaam.
Bw. Kisesa amesema kuwa, Mamlaka inatambua kwamba waongozaji ndege pamoja na kada nyingine wanahitaji kupewa mafunzo yatakayozidi kuwajengea uwezo wa utendaji na utekelezaji wa majukumu yao na hivyo Mamlaka hiyo itahakikisha inawapatia wataalam hao mafunzo thabiti yatakayoongeza weledi katika maeneo yao ya kazi.
Akizungumza kwa niaba ya waongozaji ndege, Rais wa TATCA Bw. Merkiory Ndaboya ameishukuru Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwa kuendelea kuinga mkono TATCA kwa kuboresha mazingira ya utendaji kazi na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa weledi kwa mujibu wa sheria.
Mkutano huo wa siku mbili umehudhuriwa na wanachama wa TATCA kutoka mikoa yote nchini Pamoja wawakilishi kutoka chama cha waongozaji ndege wa Uganda (UGATCA) na chama cha waongozaji ndege kutoka Comoro (IPCNA).
Rais wa Chama cha Waongozaji ndege Tanzania (TATCA), Merkiory Ndaboya akizungumza kuhusu jinsi chama hicho kilivyoweza kuwasimamia pamoja na kuwapatia elimu waongoza ndege nchini Tanzania wakati wa kufunguzi wa Mkutano wa 43 wa TATCA uliofunguliwa na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege Hamis Kisesa aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza S. Johari Novemba 24, 2023 katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wataalam wa Chama cha Waongozaji ndege Tanzania (TATCA), viongozi wa TCAA wakisikiliza hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza S. Johari iliyosomwa na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege Hamis Kisesa alipokuwa anafungua mkutano mkuu wa 43 wa Chama cha Waongozaji ndege Tanzania (TATCA) uliofanyika Novemba 24, 2023 jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege Hamis Kisesa aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza S. Johari akitoa zawadi kwa baadhi ya Waongozaji Ndege Wastaafu kwa kutambua mchango wao wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 43 wa mwaka uliofanyika Novemba 24, 2023 katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
Mwongozaji Ndege Mwandamizi Mtaafu Justine Ncheye akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Waongozaji Ndege Wastaafu kwa kutambua mchango wao wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 43 wa mwaka uliofanyika Novemba 24, 2023 katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege Hamis Kisesa aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Hamza S. Johari(aliyekaa katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waongoza ndege Tanzania waliohudhuria mkutano wa 43 wa Chama cha Waongozaji ndege Tanzania (TATCA) uliofanyika Novemba 24, 2023 jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uongozaji Ndege Hamis Kisesa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna waongoza ndege wanavyotakiwa kupewa elimu kila wakati ili kuendana na teknolojia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 43 wa mwaka uliofanyika Novemba 24, 2023 katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
Rais wa Chama cha Waongozaji ndege Tanzania (TATCA), Merkiory Ndaboya akizungumza na wandishi wa habari kuhusu malengo ya chama hicho ikiwa ni kuwaweka wanachama pamoja ili kuendana na wakati pamoja na kuwapa mafunzo wanachama hao kwenye mafunzo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 41 wa mwaka uliofanyika Novemba 26, 2021 katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.
إرسال تعليق