Katika kutekeleza majukumu yake ya Kisheria Baraza la washauri la watumiaji huduma za mawasiliano (TCRA CCC),
chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Hawa Ng'humbi
imefanya mkutano na Umoja wa Watoa Huduma za Mawasiliano (TAMNOA) kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayomhusu mtumiaji wa huduma za mawasiliano ili kuboresha huduma kwa mtumiaji.
Mkutano huo uliofanyika leo Jumatatu Novemba 27, 2023 pamoja na mambo mengine umeangazia changamoto za watumiaji na namna ambavyo TCRA CCC, Watoa Huduma na wadau wengine wanaweza kuzishughulikia ili kuondoa kero kwa watumiaji.
#HudumaBoraZaMawasilianoNiHakiYako
#TanzaniaYaKidijitali
إرسال تعليق