Na Mwandishi wetu.
BENKI ya NMB mkoa wa Geita imefanya vizuri katika mashindano ya bonanza la michezo la benki ya NMB iliyofanyika katika shule ya sekondari Chato wilayani Chato mkoani Geita.
NMB Geita imefanikiwa kushinda katika mchezo wa kuvuta kamba kwa upande wa wanaume dhidi ya benki ya NMB Kagera.
Kwa upande wa mpira wa wavu NMB Geita iliibuka na ushindi wa seti 3-0 dhidi ya NMB Kagera.
Katika mchezo wa mpira wa pete,NMB Geita ilishinda kwa mabao 10-1 dhidi ya NMB Kagera.
Kwa upande wa mpira wa miguu,NMB Kagera ilishinda kwa mabao 3-0 dhidi ya NMB Geita. Mabao ya NMB Kagera yalifungwa na Dastan Kato katika dk ya 16,Aidan Mshua katika dakika ya 34 na Gosbert Madembwe katika dakika ya 85.
Meneja wa timu ya NMB Geita,Derick Kamugisha ameipongeza timu yake kwa kufanya vizuri katika michezo mbali mbali. Kamugisha amesema watajipanga vizuri zaidi kwajili ya bonanza lijalo.
Meneja wa timu ya NMB Kagera Aidan Kanyari amesema bonanza hilo limewasaidia katika kuendeleza umoja katika michezo baina ya wafanyakazi wa NMB Geita na NMB Kagera.
Ameuomba uongozi wa benki ya NMB Kanda ya Ziwa bonanza hilo liwe endelevu.
Naye meneja wa benki ya NMB Kanda ya Ziwa Wogofya Mfalamagoha amepongeza wafanyakazi wa benki ya NMB kutoka mikoa ya Kagera na Geita kwa kushiriki katika bonanza hilo.
Amesema wafanyakazi wa benki ya NMB wanatakiwa kuandaa timu za mikoa kupitia benki yao kisha kuandaa timu ya Kanda itakayokuwa imara kwajili ya kushindana na kanda zingine za benki ya NMB.
إرسال تعليق