BUNGE SC - SOKA (TULIA BOYS) YAIBURUZA KENYA BAO 4-1


Magoli yaliyofungwa na Jafary Chege (Rorya),  Simai Hassan (Nungwi), Cosato Chumi Gaza (Mafinga Mjini) na Ramadhan Billa (Chakechake) yametosha kunogesha Miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara baada ya Bunge SC -Soka kuwachapa Bunge la Kenya kwa mabao 4-1 katika mchezo mkali na wa kuvutia Kwenye Uwanja wa Pele Kigali.

Akizungumza leo na Fichuzi Blog Captain Bunge SC - Soka
Mhe. Cosato Chumi wakati akitoa taarifa juu ya kile kinachoe ndelea katika uwanja wa Pele Kigali  amesema Ushindi huo umefanya Bunge SC -Soka maarufu kama Tulia Boys kuongoza kwa kuwa na point tatu, wakifuatiwa na Bunge la Afrka Mashariki -EALA na Wenyeji Bunge la Rwanda ambao walitoka suluhu katika mechi ya ufunguzi .

Katika hatua nyingine mapema leo mchezo kati ya Bunge la Uganda na Sudan Kusini haukuweza kufanyika baada ya kila timu kutuhumu kwamba kuna wachezaji ambao sio Wabunge kinyume na Kanuni ya Michezo inayotaka Washiriki kuwa Wabunge tu.

Akiendelea kutoa ufafanuzi wa kinachoendelea amesea kesho ambayo ni siku ya tatu ya Michezo hiyo ya 13 ya Mabunge ya Afrika Mashariki itakuwa siku ya mchezo wa Riadha .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bunge Sports Club Mhe. Abbas Tarimba amewapongeza wachezaji wa Bunge SC -Soka (Tulia Boys) kwa ushindi huo mnono huku akieleza matamanio yake yalikuwa wafunge magoli 5-1, akikumbukia November 5.
 
Endelea kuwa karibu na Fichuzi Blog kwa mwendelezo wa taarifa mbalimbali ikiwemo yanayoendelea kujiri katika ukanda wa kimichezo kutoka katika uwanja wa Pele Kigali.
 





Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA