ELIMU YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA YA JESHI LA POLISI NA BARRICK YAENDELEA KUWAFIKIA WANAFUNZI MKOANI DAR ES SALAAM

Wanafunzi wakifuatilia mafunzo ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia yanayotolewa na Askari kutoka Jeshi la Polisi katika madawati ya kijinsia.
Mkufunzi wa Chuo Cha Polisi Kurasini, Dawati la Jinsia na Watoto,SSP Moses Mpongo akitoa mafunzo juu ya madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Uhamiaji wakati wa mafunzo ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.

****

Wakati maadhimisho ya Siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia yakiendelea nchini na duniani kote, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na kampuni ya Barrick, linaendelea kufikisha elimu ya vitendo hiyo katika shule mbalimbali katika mkoa wa Dar es Salaam,kupitia kwa Maofisa Waandamizi wa Polisi ambao wamebobea kutoa mafunzo haya kwa nadharia na vitendo.

Shule ambazo Maofisa kutoka Jeshi la Polisi tayari wamefikisha elimu hiyo ni shule ya msingi Kawe A,Sekondari ya Daniel Chongolo ,Sekondari ya Uhamiaji na shule ya msingi Mbezi Beach. Mafunzo haya yataendelea kufikia shule mbalimbali za msingi na sekondari na kwenye jamii zenye mikusanyiko ya watu wengi kwenye kipindi hiki cha maadhimisho hayo.
Mkuu wa Polisi,Kitengo cha Dawati la Jinsia kata ya Kawe,ASP Elizabeth Msabira akitoa zawadi kwa wanafunzi waliojibu vizuri wakati wa mafunzo ya elimu ya kupinga vitendo vya ukatili katika shule ya msingi Tumaini.
Wanafunzi wakifuatilia mafunzo ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia yanayotolewa na Askari kutoka Jeshi la Polisi katika madawati ya kijinsia.
Wanafunzi wakifuatilia mafunzo ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia yanayotolewa na Askari kutoka Jeshi la Polisi katika madawati ya kijinsia.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Uhamiaji iliyopo Temeke wakifuatilia mafunzo kuhusu ukatili wa kijinsia.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Uhamiaji iliyopo Temeke wakifuatilia mafunzo kuhusu ukatili wa kijinsia.
Wanafunzi wa shule ya Tumaini, Kawe, wakisikiliza mafunzo ya Kupinga ukatili wa kijinsia iliyotolewa na wataalamu wa masuala ya jinsia kutoka Jeshi la Polisi.
Wanafunzi wa shule ya Tumaini, Kawe, wakisikiliza mafunzo ya Kupinga ukatili wa kijinsia iliyotolewa na wataalamu wa masuala ya jinsia kutoka Jeshi la Polisi.
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Tumaini, iliyopo Kawe jijini Dar es Salaam,Seleman Ally (mwenye fulana nyeupe) akishirikiana na wataalamu kutoka Jeshi la Polisi kuwapatia wanafunzi elimu ya kupinga vitendo vya Ukatili wa kijinsia.
Waendeshaji wa elimu ya ukatili wa kijinsia kutoka Jeshi la Polisi walibadilishana mawazo na Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Tumaini iliyopo Kawe jijini Dar es Salaam,SelemanAlly (wa pili kutoka kushoto)kabla ya kuanza mafunzo.
Wanafunzi wa kike kutoka shule ya Tumaini, Kawe wakiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Polisi baada ya kupatiwa mafunzo ya kupinga vitendo vya Ukatili wa kijinsia na kupatiwa zawadi ya taulo za kike.
Wanafunzi wa shule ya Tumaini, Kawe, wakisikiliza mafunzo ya Kupinga ukatili wa kijinsia iliyotolewa na wataalamu wa masuala ya jinsia kutoka Jeshi la Polisi.

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA