MTOTO WA MIEZI 9 ANUSURIKA KIFO, TUKIO LA KUSHANGAZA WAKATI WA UOKOAJI HANANG


Kufuatia mafuriko yanayoendelea Hanang Mkoani manyara yaliyosomba magari, miti na magogo limetokea tukio la kushangaza la kupatikana kwa mtoto mwenye umri wa miezi 9 akiwa hai licha ya kusombwa na maji hayo wakati wa shughuli za uokoaji zikiendelea.

Wakizungumza leo Mkoani Manyara Mashuhuda waliokuwemo katika eneo hilo akiwemo Bwn. Rajab Hussein, Bwn. Emmanuel na Bwn, Joshua wametanabaisha hali halisi kwa kile walichokishuhudia ikiwa ni pamoja na kufanya shughuli za uokoaji pale msaada ulipohitajika na kwamba mtoto huyo alikutwa akiwa amebanwa kwenye gogo pembeni ya gari la mafuta katika kituo Cha kuwekea mafuta Katesh na hatimaye walifanikiwa kumwokoa.
 "Mtoto wa miezi tisa alinasa pale kwenye gari la mafuta gafla tukasikia sauti ya mtoto analia tulipoenda kumwangalia tukamkuta yuko hai na baadaye wazazi wake waliposikia mtoto ameokolewa maeneo ya sheli wakamfata mtoto wao na hatimaye wakampeleka kwenye hospitali ya Tumaini" Alisema Shuhuda huyo
 
Wakati shughuli za uokoaji zikiendelea tukio lingine katika mazingira ya kushangaza ni mama aliyekuwa na watoto wake wawili mmoja akiwa amemweka mbele na mwingine mgongoni ambapo mama na yule mtoto wa mbele alifariki baada ya kunasa kwenye matope lakini mtoto aliyekuwa mgongoni alibaki salama sababu kubwa ikitajwa kuwa alikuwa anaweza kupumua vizuri na hatimaye wakaweza kumwokoa mtoto huyo!

"Inaonekana yule mama alizidiwa na tope akiwa anamtoto amemshikilia mkononi na mwingine akiwa mgongoni, yule mtoto aliyekuwa mgongoni alikuwa anapata hewa na tulifanikiwa kumwokoa lakini kwa bahati mbaya mama na yule mtoto aliyekuwa amemshikilia mbele walifariki kwa kukosa hewa" Amesema shuhuda huyo

"Kuna maiti zingine zilikuwa zinakuja na maji tukazizuia licha ya kushindwa kusaidia wote kwani Kuna wengine walikuwa ndani na hatukuweza kuwapa msaada na hata haya magari hayakuwa hapa yamesombwa na mafuriko yakajakutwama hapa". Amesema shuhuda huyo


Vifo mafuriko Manyara vyafikia 23, majeruhi 30 - HabariLeo

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA