MWENYEKITI WA BODI YA NSSF AFANYA ZIARA YA KIKAZI MAKAO MAKUU YA NSSF




*Aahidi ushirikiano wa kutosha kufanikisha utendaji wa Mfuko


*Mkurugenzi Mkuu aweka wazi mafanikio na mikakati ya uboreshaji huduma

Na MWANDISHI WETU

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bi. Mwamini Malemi, amefanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) jijini Dar es Salaam, na kuahidi kufanya kazi kwa ushirikiano na Menejimenti pamoja na wafanyakazi wa Mfuko.

Katika ziara hiyo ya kikazi iliyofanyika  tarehe 5 Desemba 2023, Bi. Malemi alikutana na kuzungumza na wajumbe wa Menejimenti ya NSSF, ambapo pamoja na mambo mengine alipokea taarifa ya utendaji kazi kutoka kwa Mkurugenzi wa Mkuu, Bw. Masha Mshomba.

Taarifa ya NSSF iliyowasilishwa na Bw. Mshomba ilionesha utendaji mzima wa Mfuko, ikigusia uandikishaji wanachama, uchangiaji, uwekezaji pamoja na ulipaji mafao. Aidha Bw. Mshomba alizungumzia kuhusu uboreshaji huduma kwa wanachama, uboreshaji mifumo na namna wafanyakazi wanavyoshirikiana katika kuhakikisha majukumu ya Mfuko yanakamilika.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzungumza na Menejimenti ya NSSF, Bi. Mwamini alimshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua kushika nafasi hiyo, ambapo aliahidi kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuweza kufikia malengo na matarajio ya Mfuko.

Awali, Bw. Mshomba alimueleza Mwenyekiti huyo matarajio ya Mfuko ikiwemo kuendelea kuboresha huduma kwa wanachama kupitia njia mbalimbali ikiwemo ya matumizi ya TEHAMA kwani hicho ndio kipaumbele muhimu cha NSSF.

Bw. Mshomba alisema matarajio ya Mfuko ni kuona mwanachama baada ya kustaafu na kuwasilisha taarifa zake zote zinazotakiwa kwa mujibu wa Sheria analipwa stahiki zake ndani ya muda mfupi.


Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA