Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akionesha misaada ya kibinadamu iliyotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka Mlima Hanang' katika wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akikabidhi sehemu ya nguo zilizotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka Mlima Hanang' katika wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi, katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amekabidhi misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula, nguo na vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka Mlima Hanang' katika wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita amekabidhi misaada hiyo leo tarehe 22 Desemba, 22,2023 kwa Mkuu wa wilaya ya Hanang Mhe. Janeth Mayanja.
Akizungumza wakati wa kukabidhi misaada hiyo, Mhe. Mndeme amesema WanaShinyanga wanaungana na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa pole kutokana na janga lililotokea Hanang lililosababishwa mvua kubwa iliyoambana na tope, mawe na miti hivyo kupelekea vifo, mali kupotea, mifugo kufa, mashamba kuharibika, nyumba kuharibika.
"Sisi wana Shinyanga tukiwa sehemu ya Watanzania tulipoguswa na janga hili tulipokea kwa masikitiko makubwa, baada ya kupokea taarifa hii ya kusikitisha, wanashinyanga kwa mapenzi mema wakaona nao wamuunge mkono Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan lakini vile vile wawaunge mkono wananchi wengine kutoa pole kwa wananchi wa Hanang hivyo tumefika hapa katika mji huu wa Katesh kuwasilisha kwako mhe. DC pole zetu ili kuonesha mshikamano, umoja na kwamba tuko pamoja katika kipindi hiki kigumu ambapo kwa wenzetu wa Hanang wanapitia",amesema Mhe. Mndeme.
"Kwa niaba ya wananchi wa Shinyanga ambao wamejitolea kutoa pole zao kwa ndugu zao wa Hanang, naomba nikakibidhi mifuko 1000 ya saruji, mchele kilo 700, unga wa mahindi kilo 355, unga lishe kilo 250,juisi katoni 500, chumvi pakti 90,sukari kilo 25,sabuni katoni 13,mafuta ya kula lita 5, viatu pea 43, nguo balo 30 kati ya balo hizo 27 zina nguo za wanaume na tatu nguo mchanganyiko”, amesema
“Misaada hii inatoka kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga ambao wamejitolea kwa mapenzi yao mema, wameguswa kwa namna moja au nyingine. Poleni sana wan Hanang, pole sana Mhe. Rais Samia, tuendelee kumuomba Mungu atuepushe na majanga haya, mvua tunaihitaji, tunaumuomba Mungu atuletee mvua yenye neema. Msaada tuliotoa ni mdogo ukilinganisha na madhara yaliyotokea tunaomba hiki kilichotolewa na wana Shinyanga mkipokee”,ameongeza Mhe. Mndeme.
Akipokea misaada hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mhe. Janeth Mayanja amewashukuru Wana Shinyanga kwa upendo,huruma, utu, ubinadamu na undugu wa kweli waliouonesha kwa wan Hanang akisisitiza pia wamemuunga mkono kwa vitendo mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
“Tunawashukuru sana Wana Shinyanga kwa misaada ya kibinadamu mliyotupatia, mmeongeza nguvu Hanang na vifaa hivi vya ujenzi mlivyotoa vitasaidia katika ujenzi wa makazi ya waathirika wa janga lililotokea”,amesema.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (kulia) akimpa pole Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara Mhe. Janeth Mayanja kufuatia janga la mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka Mlima Hanang'. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati akikabidhi misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula, nguo na vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka Mlima Hanang' katika wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati akikabidhi misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula, nguo na vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka Mlima Hanang' katika wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati akikabidhi misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula, nguo na vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka Mlima Hanang' katika wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akikabidhi sehemu ya nguo zilizotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka Mlima Hanang' katika wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi, katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara Mhe. Janeth Mayanja akitoa neno la shukrani kwa wananchi wa Shinyanga

Awali Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi, (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita wakikagua mzigo walioleta Hanang'
Muonekano wa magari yaliyobeba misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula, nguo na vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka Mlima Hanang' katika wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita wakitembelea moja ya maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko wilaya ya Hanang'
Katibu Tawala Wilaya ya Hanang' Mwl. Athuman Likeyekeye akiwaonesha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme ,Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita wakitembelea moja ya maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko wilaya ya Hanang'
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme( katikati) Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi (wa pili kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita wakiwa katika eneo la Jorodom moja ya maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko wilaya ya Hanang'
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiangalia miongoni mwa mawe yaliyosukumwa na maji kutoka Mlima Hanang' hadi katika eneo la Jorodom moja ya maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko wilaya ya Hanang'
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiangalia miongoni mwa miti iliyosukumwa na maji kutoka Mlima Hanang' hadi katika eneo la Jorodom moja ya maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko wilaya ya Hanang'
إرسال تعليق