SERIKALI KUIMARISHA UKUSANYAJI MAPATO, MBUNGE AIBANA SERIKALI KUJA NA TAKWIMU


                              Na, Mwandishi wetu - Dodoma.
 
Serikali inatambua ufinyu wa bajeti za kufuatilia miradi hususani katika ngazi za Kata na Vijiji kutokana na ufInyu wa bajeti hivyo itaendelea kuimarisha ukusanyaji wa mapato ili kuongeza bajeti ya usimamizi wa miradi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kote Nchini.
 
Ni kufuatia swali la msingi la Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mhe.Mwita Mwikwabe Waitara alilouliza kuwa "Je, kwa nini Serikali haitengi fedha za kufuatilia Miradi ya Maendeleo kwa ngazi za Kata na Vijiji?." 
Akijibu swali hilo Naibu waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Deogratius Ndejembi amebainisha kuwa ni kweli serikali inatambua umuhimu wa ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo katika ngazi za msingi ili kuongeza ufanisi na tija katika miradi inayotekelezwa.
 

"Miradi inayotekelezwa katika Vijiji na Kata husimamiwa na viongozi na wataalam/watendaji wa ngazi zote za Serikali kuanzia Taifa, Mikoa na Halmashauri, Kata na Vijiji/mitaa. Gharama za ufuatiliaji wa miradi hii hutokana na bajeti za Serikali za usimamizi wa miradi kutokana na fedha za matumizi mengineyo (OC) na fedha za mapato ya ndani katika Halmashauri." Amesema Ndejembi
 
 
Kufuatia majibu hayo ya Serikali yakamfanya Mbunge  Waitara kuongeza swali la nyongeza alilotaka kujua takwimu katika Majimbo kama viongozi wa chini katika ngazi ya vijiji kama kuna waliowahi kulipwa chochote ambao wapo katika kamati iliyoundwa na wananchi katika sekta ya ujenzi, mapokezi na manunuzi.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri Ndejembi amesema kuwa jukumu na mamlaka ya kuweza kusimamia ujenzi wa miradi mbalimbali katika halmashauri ni halmashauri yenyewe.

"Hii miradi inayoletwa ya vituo vya afya, Shule n.k ni 'Complimentary' kutoka serikali kuu Lakini mamlaka na wajibu wa halmashauri kuendana na dhana ya 'D by D' ni wao wenyewe kuweza kukusanya mapato yao na kuweza kupanga miradi yao ya maendeleo kutenga fedha hizi, katika miradi hii ambayo inatoka serikali kuu fedha ya 'Monintary' ipo Mkoani na inapelekwa Wilayani" Amesema Naibu Waziri Ndejembi 

Ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa kutoa wito kwa wakurigenzi wote Nchini kuendelea kuishi dhana ya 'D by D' na kutenga fedha ya ufuatiliaji kwenye miradi ya maendeleo ambayo inaletwa na serikali kuu kwa kutenga fedha kutoka kwenye mapato yao ya ndani ili hizi kamati ambazo zipo walau waweze kupata maji ya kunywa kipindi Cha usimamizi wa miradi hiyo.

"Kuhusu takwimu tutafuatilia katika halmashauri zetu kwenye Ile dhana ya ugatuaji wa madaraka, tutafuatilia na kuona ni halmashauri zipi ambazo zilitenga fedha hizi na tutaleta mbele ya bunge hili tukufu" Amesema Ndejembi.
 


Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA