BENKI YA CRDB KANDA YA MAGHARIBI YAZINDUA KAMPENI YA AMKA NA CRDB MTAANI KWAKO

Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa na mabango yaliyoandikwa West is the Best wakati Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi ikizindua Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa na mabango yaliyoandikwa West is the Best wakati Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi ikizindua Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako

Na Kadama Malunde- Malunde 1 blog

Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi imezindua Kampeni yake mpya iitwayo Amka na CRDB Mtaani Kwako inayolenga kuwafikia wateja wengi zaidi ambao walikuwa hawana elimu kuhusu benki ya CRDB na hawajajiunga na benki hiyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo ya Amka na CRDB Mtaani Kwak oleo Jumanne Januari 23,2024 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Ndg. Jumanne Wambura Wagana amesema Kampeni hiyo itafanyika kwa siku 22 ndani ya mikoa minne ya Shinyanga, Geita, Kigoma na Tabora.

Amesema Kampeni hiyo imelenga kuamsha (Amka na CRDB) wateja wote wa Kanda ya Magharibi wakiwemo wafanyabiashara, wakulima, Watumishi, Wastaafu, Wachimbaji wa madini, Wanafunzi na hata watoto wadogo ambao walikuwa hawajajiunga na huduma za CRDB.

“Kampeni hii imelenga kuwafikia wateja wa Benki ya CRDB popote walipo mtaani, wale ambao bado hawajajiunga na familia ya CRDB wajiunge na huduma za CRDB, tunaenda kuwaamsha na kuwaleta wajiunge na CRDB kwa sababu bado kuna watu wengi hawajajiunga na huduma za CRDB inawezekana hawana elimu kwa hiyo tutapita mtaa kwa mtaa, nyumba kwa nyumba, barabara kwa barabara , mahali pote penye watu wengi kanda yote ya Magharibi”,ameeleza Wagana.
“Kupitia kampeni hii tutapita mtaa kwa mtaa wilaya kwa wilaya ndani ya mikoa minne ya Kanda ya Magharibi kutoa elimu ya bidhaa za CRDB ambapo wateja wengi wataweza kufungua akaunti kwa masharti nafuu kabisa ikiwemo kuwa na namba NIDA pekee inatosha kufungua akaunti na kama hauna basi kitambulisho chochote kinachotambulika kama Kitambulisho cha Mpiga kura, Leseni ya Udereva , Pasipoti ya kusafiria n.k.”,ameeleza Wagana.

Amesema pia watatoa huduma zingine kama Mikopo, Huduma za Bima, Huduma kuunganishwa Kidigitali ikiwemo Sim Banking, kusimika Mawakala wapya na vituo vya Malipo na huduma zingine nyingi.

“Tuna Matawi 25 Kanda ya Magharibi, na tunayo timu yetu ya Freelancers ambao wapo kila tawi ndiyo wanahusika kupeleka ujumbe wa Benki ya CRDB na kutuletea wateja wengi zaidi kuweza kufikia mafanikio yetu ya Benki. West is The Best, Ulipo Tupo”,amefafanua.

“Tunataka kupeleka ujumbe na bidhaa zetu kwa wateja kule kule walipo lakini na kuwaambia kuwa CRDB Wakala ipo kule mtaani wanaweza kupata huduma za Kibenki ikiwemo kufungua Akaunti, kuweka fedha, kutoa fedha, kulipa Bili za serikali n.k”,ameongeza Wagana.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Ndg. Jumanne Wambura Wagana akizungumza wakati akizindua Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako leo Jumanne Januari 23,2024 katika Benki ya CRDB tawi la Shinyanga- Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Ndg. Jumanne Wambura Wagana akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Ndg. Jumanne Wambura Wagana akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Ndg. Jumanne Wambura Wagana akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Ndg. Jumanne Wambura Wagana akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Ndg. Jumanne Wambura Wagana akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa na mabango yaliyoandikwa West is the Best wakati Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi ikizindua Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakiwa na mabango yaliyoandikwa West is the Best wakati Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi ikizindua Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakipiga picha ya kumbukumbu wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako

Burudani ikiendelea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako

Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Amka na CRDB Mtaani Kwako.

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA