WANAFUNZI WALIOTINGA KWA MTENDAJI NA BARUA HAWATAKI SHULE, SERIKALI YASIMAMA KIDEDEA

 MARA.


Wanafunzi wawili wa Kijiji cha Bwitengi Wilaya ya Serengeti waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Ikoma Sekondari mwaka huu wametinga kwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Manchira na barua kuwa hawataki kusoma.


Watoto hao wenye umri wa miaka (15) majina yao tunayo siku ya Jumatano Januari 10,2024 majira ya asubuhi wakiambatana na wazazi wao waliwaasilisha barua hizo.


Katika barua zao ambazo Serengeti Media Centre na Antoma Tv Online imefanikiwa kuziona,wanadai kuwa hawana akili ya kusoma na hivyo mmoja anataka akafanye biashara na mwingine akalime.


Mbele ya Ofisa Mtendaji wa Kata ya Manchira Loshilaa Ole walishikilia msimamo wao kuwa hawawezi kusoma kwa kuwa uwezo wa akili yao umefikia hapo.


Hata walipofikishwa kwenye dawati la Jinsia Kituo cha Polisi Mugumu mbele ya wazazi walishikilia msimamo huo,hata hivyo baada ya kuwatenga na kuwabana walikubali kuanza masomo na kudai shinikizo lilitoka kwa wazazi wao ambao hawakutaka kuwanunulia mahitaji.

“Watoto kwa nyakati tofauti walisema,mmoja baba yake alishafariki akaacha ng’ombe,mama hakutaka kuuza amnunulie mahitaji ikabidi amwambie mwanae namna ya kukwepa,ili kuongeza nguvu naye akatafuta rafiki yake ambaye mzazi wa kiume hayupo hapo kijijini naye hajatuma mahitaji,”amesema mtoa taarifa.


Amesema,walikubali kuanza masomo na wazazi wakaagizwa wawanunulie mahitaji,”nadhani jana Januari 11,2024 wazazi walienda mnadani kuwanunulia mahitaji,hawa watoto wote wamesoma Bwitengi shule ya msingi na wana uwezo mzuri,ilitushangaza kudai akili zao zimeishia hapo,”amesema.


Kija Nyamoronga Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Marafiki wa Elimu Serengeti (MESE)amesema”nililazimika kufuatilia ofisi ya kata ikaonekana wana msimamo nikashauri wafikishwe dawati la polisi ili tujue nyuma ya uamzi wa hawa yupo nani,maana wangeachwa hawa , kuambukiza wengine,”amesema.


Amewaomba wazazi kuacha tabia za kushirikiana na watoto kwa mambo ambayo hayana faida kwa kuwa watakuja juta baadae.


Elimu ya sekondari humuandaa mtoto kukabiliana na changamoto za maisha.Hakikisha mtoto anaripoti shuleni kuanza kidato cha kwanza kwa wakati.

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA