WATU 25 WAFARIKI DUNIA KWENYE AJALI ARUSHA


1000605030

Na. Abel Paul, Jeshi la Polisi- Arusha.

Watu ishirini na tano (25) wameafariki dunia huku wengine ishirini na moja (21) wakijeruhiwa katika ajali iliyotokea maeneo ya Ngaramtoni kibaoni by Pass ikihusisha Lori na magari mengine madogo matatu Wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha.

Akitoa taarifa ya ajali hiyo Kamishna wa Polisi Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi CP Awadhi Juma Haji alipofika katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru amesema ajali hiyo ilitokea Februari 24,2024 muda wa saa 11:00 jioni katika Barabara ya Arusha Namanga ambapo ilihusisha lori lenye namba za usajili KAC 943 H aina ya Mack lenye tela namba za usajili ZF 6778 mali ya kampuni ya KAY Construction ya Nairobi Nchini Kenya.

1000605032

CP Awadhi ametaja idadi ya waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni wanaume (14) wanawake (10) na mtoto mmoja wa kike ambao jumla yao ni (25) huku akiitaja idadi ya raia wa kigeni waliofariki kuwa ni saba (07).

Katika ajali hiyo pia CP Awadhi ametaja idadi ya majeruhi kuwa ni 21 kati yao wanaume ni kumi na nne (14) na wanawake ni saba (07), huku akitaja magari yaliyopata ajali katika tukio hilo kuwa ni T 623 CQF aina ya Nissan Caravan, T 879 DBY aina ya Mercedes Benz Saloon na gari namba T 673 DEW aina ya Toyota coaster mali ya shule ya (New Vision School).

Pia kamishna huyo wa opereshini na mafunzo ya Jeshi la Polisi nchini amekitaja chanzo cha ajali hiyo kuwa kuwa ni kufeli breki ya lori kitendo kilichopelekea lori hilo kuyagonga magari mengine yalikuwa mbele yake huku akibainisha kuwa Jeshi hilo linaendelea kumtafuta dereva aliyesababisha ajali hiyo ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.


1000605031

Sambamba na hilo ametoa Pole kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha na watanzania kwa ujumla na raia wa kigeni waliopoteza ndugu zao katika ajali hiyo.

1000605029
IMG-20240225-WA0043
IMG-20240225-WA0045
IMG-20240225-WA0046
IMG-20240225-WA0042
IMG-20240225-WA0041
IMG-20240225-WA0028
IMG-20240225-WA0030
IMG-20240225-WA0039
IMG-20240225-WA0029

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Jumanne Sagini leo februari 25,2024 amewatembelea na kuwajulia hali majeruhi wa ajali katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Arusha Mount Meru Arusha ambapo iliyohusisha Lori na magari mengine matatu na kupelekea vifo 25 na majeruhi 21.

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA