BARABARA ILIYOPOTEZA MAWASILIANO KWA SAA 17 YALIZA ABIRIA, BASHUNGWA AFUNGUKA MAZITO



 Na, Mwandishi wetu - Dar Es Salaam.

Serikali wamefanikisha kutatua changamoto ya kukatika kwa daraja la somanga lililokatisha mawasiliano tokea jana machi 24,2024 kutokana na athari za mvua zinazoendelea kunyesha kwenye maeneo tofauti katika mikoa ya kusini.


Daraja hilo linaunganisha mkoa wa dar es salaam na mikoa ya kusini Pwani, lindi na mtwara ndilo linalobeba uchumi wa mikoa hiyo kwani hakuna barabara nyingine inayounganisha mikoa hiyo kiuchumi.


Wananchi wamekuwa wakilalamikia gharama kubwa za kujikimu zilikuwa wakizifanya ili kupata mahitaji yao ya kawaida kwa kipindi chote cha kusubiri.


"Hapa tulipo kwenda kutafuta mahitaji yetu kama chakula tukichukuwa bodaboda tunatumia elfu 3, pesa ambayo haikuwa kwenye bajeti yangu na ukiangalia maisha yenyewe ya sasa tumeteseka sana lakini pia Mwandishi kitu ambacho ni cha ajabu tumejisaidia maporini sababu kwanza hadi tufike kwenye makazi ni mbali sana na gharama kubwa." Alisema Jumanne

 

Aidha Amina Yusuph aliyekuwa akisfiri kutoka Dar es salaam kwenda mtwara yeye amewalalmikia wakaziwa hapo kwa kupandisha bei za bidhaa mbalimbali


"Tumefika hapa tokea jana majira ya saa 2 usiku kila kitu wenyeji wetu walikifanya kuwa ni fulsa sababu wemetuongezea bei za vyumba vya wageni mwanzo walikuwa wanafanya elfu 10 hadi elfu 15 ila sisi tumelipia elfu 20 hadi elfu 30" alisema Amina Yusuph


Aidha baadhi yao wameipongeza serikali kwa juhudi kubwa walizozifanya kwa kuhakikisha wanarekebisha na kuruhusu eneo hilo ili shughuli za barabara hiyo ziendelee.

Awali timu ya wataalamu kutoka Wakala wa Barabara (TANROADS) mkoa wa pwani na Lindi waliungana ili kurejesha mawasiliano ya barabara katika eneo la Somangafungu Mkoani Lindi kutokana na daraja hilo linalounganisha barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam na Mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara kukatika na kusababisha barabara hiyo kufungwa.


Akitoa taarifa Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa jitihada kubwa zimefanyika za kurudisha mawasiliano ya barabara eneo la Somangafungu, Lindi. 


“Timu za TANROADS kutoka Mikoa ya Lindi na Pwani zimeungana kuongeza nguvu ili kabla ya mchana safari ziweze kuendelea. Tunawapa pole wasafiri wote kwa changamoto iliyojitokeza”, ameeleza Waziri Bashungwa.

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA