Watumishi watano wa Kituo cha Afya Mikanjuni wamesimamishwa kazi kufuatia kifo cha mjamzito Fatuma Mussa Suleiman (36) mkazi wa Magaoni Jijini Tanga aliyefika kituoni hapo kwa ajili ya kujifungua na inadaiwa kuwa wahudumu wa zamu walifanya uzembe kwa kumuwekea damu ambayo hakustahili wala hakuwa na uhitaji nayo
Akitoa taarifa ya Serikali, Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe. James Kaji amesema baada ya kutokea uzembe kwa marehemu kuwekewa damu ambayo hakuwa na uhitaji nayo alipata uzio mkali (Allergic Reaction) na kisha kupelekea kifo chake.
"Mgonjwa alifanyiwa upasuaji ambapo alifanikiwa kupata mtoto wa kike na hakukuwa na changamoto yoyote kwa mama wala kwa mtoto baada ya upasuaji na aliendelea na matibabu chini ya uangalizi wa madaktari na wauguzi wa zamu."
"Katika wodi hiyo alipolazwa kulikuwa na mgonjwa ambaye alikuwa na uhitaji wa kuwekewa damu na ilikuwa tayari imeandaliwa, kwahiyo muuguzi aliyekuwa zamu alimwekea damu marehemu baada ya mgonjwa aliyekuwa anatakiwa kuwekewa damu" amesema DC James Kaji
Aidha, amewataja watumishi waliosimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tukio hilo ni pamoja na wauguzi watatu ambao ni Fadhila Ally Hoza, Restituta Kasendo Deusdedit, pamoja na Muya Ally Mhando ambapo kwa upande wa madaktari ni Hamis Mohamed Msami pamoja na Andrew Eliasikia Kidee.
إرسال تعليق