DHANA ILIYOPELEKEA KUANZISHWA KWA WAKALA WA TAIFA WA HIFADHI YA CHAKULA (NFRA)



Kanzishwa kwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ni kutokana na tatizo la ukame lililojitokeza miaka ya 1973 - 1975 wakati Tanzania ilipopata athari kubwa ya upungufu wa chakula hivyo kushindwa kumudu mahitaji ya ndani ya chakula na kulazimika kuagiza chakula kutoka nje ya nchi. 

Hali hiyo ilisababisha Serikali kuanzisha Hifadhi ya Chakula ya Taifa (Strategic Grain Reserve - SGR) mwaka 1976 ikiwa ni mbinu ya kuiwezesha kuepuka au kupunguza makali ya upungufu wa chakula nchini. 

Kutoka kipindi hicho SGR ilifanyiwa mabadiliko mbalimbali ya kimuundo na uwajibikaji. NFRA iliundwa kuchukua majukumu wa SGR ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa jukumu.


Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula - National Food Reserve Agency (NFRA) ni Taasisiya Umma iliyo chini ya Wizara ya Kilimo. Wakala ulianzishwa kwa Sheria ya Wakala za Serikali Sura 245 (Na. 30/1997), kama ilivyorekebishwa na Sheria namba 13 ya mwaka 2009, ikisomwa pamoja na Hati Rasmi iliyoanzisha NFRA mwaka 2008 kupitia Tangazo la Serikali Na. 81 la tarehe 13 Juni, 2008 na kuhuishwa na Tangazo la Serikali Na. 120 la mwaka 2016.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula Dkt . Andrew Marceline Komba akiwa kwenye kipindi cha Good Morning cha Wasadi Fm ameongelea mambo mbalimbali pamoja na mwenendo wa Hali ya Chakula Nchini.




Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA