HALMASHAURI YA TARIME YAPONGEZWA KWA MATUMIZI MAZURI YA FEDHA ZA UJENZI


                          Na, Mwandishi wetu - Mara.

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), imeipongeza Halmashauri ya Mji wa Tarime kwa matumizi mazuri ya fedha katika ujenzi wa mradi Jengo la Utawala la Halmashauri hiyo.


Kauli hiyo imetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Mheshimiwa Stansalaus Mabula wakati Kamati alipotembelea mradi huo pamoja na Mradi wa Ujenzi wa Soko la Kisasa katika Halmashauri hiyo.


Alisema Jengo hilo ni zuri ukilinganisha na majengo mengi ambayo Kamati imeshayatembelea na kuyakagua.


"Kamati inatoa pongezi kwa namna mlivyotumia fedha vizuri ambazo zimesaidia kujenga uzio, kibanda cha mlinzi na kukunua baadhi ya samani na bado mmebakiza Shilingi Milioni 82," alisema.


Aidha, alisema Kamati inaelekeza Halmashauri hiyo kuzingatia taratibu zote katika kila hatua ya utekelezaji wa mradi kuanzia ngazi ya manunuzi pamoja na kujibu hoja za kiukaguzi zilizojitokeza na kuziwasilisha.


Kuhusiana na mradi wa soko, Mheshimiwa Mabula alisema Kamati inaelekeza mradi ukamilike kwa wakati kwa kuwa muda umeshaongezwa kwa zaidi ya mara nne nje ya mkataba.


"Mjitahidi huu muda wa tarehe 17 Mei, 2024 uwe muda mwisho wa kukamilisha mradi kwa kuwa fedha iliyotumika katika ujenzi wa mradi huu haitakuwa na thamani kama mradi hautakamilika," alisema.


Alielekeza pia Halmashauri kupanga vizuri bei za vizimba kwa kufanya utafiti vizuri.




Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA